Baada ya kupokea barua kutoka kwa Mkurugenzi wa tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) iliyomteua ndugu Fatuma Ngozi kuwa diwani mpya wa viti maalumu kutoka Chama cha Wananchi(CUF), Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani bi betarice Dominic amefanya hafla fupi ya kumupisha diwani huyo.
Akizungumza kwenye zoezi hilo lililofanyika Juni 8, kwenye ukumbi wa Mikutano wa Manispaa Hakimu mkazi wa mahakama Elizabeth Misana amemueleza diwani huyo kuwa baada ya kula kiapo anatakiwa akatekeleze majukumu yake kwa kufuata sheria na bila kuangalia itikadi za chama
Aidha hakimu huyo amemtahadaharisha diwani kuwa endapo atakiuka na akashindwa kutekeleza mambo kwa mujibu wa sheria, kutokuwa na maadili na kushindwa kusimamia kanuni za halmashauri atalazimika kujipelekea mwenyewe mahakamani kwa kuwa ni kosa la jinai au atalazamikika kulipa fidia .
Kwa upande wake Mstahiki Meya wa Manispaa Mhe. Geofrey I.Mwanichisye amemtaka diwani huyo kuvifanyia kazi vitendea kazi atakavyokabidhiwa na mkurugenzi na kumtaka kufanya kazi kwa bidii kwani kuteuliwa kwake iwe faraja kwa maendeleo ya Manispaa na kumtaka kutoingia kwenye vikundi vilivyo na nia ya kuivunja Manispaa.
Bi betarice Dominic Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani amemkaribisha diwani huyo ndani ya Manispaa na kumuahidi kumpa ushirikiano pale inapobidi.Aidha amemkabidhi vitendea kazi diwani ikiwa ni pamoja na Kanuni za kudumu za halmashauri, kitabu cha maadili cha madiwani pamoja na kitini cha majukumu ya madiwani.
Uteuzi wa Mhe Fatma Ngozi umefanyika kuchukua nafasi ya Mhe Swahiba Mkauja aliyekuwa diwani kwa wakati huo baada ya kufariki Novemba mwaka jana.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.