Baraza la Wafanyakazi Manispaa ya Mtwara-Mikindani kwa pamoja limeridhia kuanzisha Mfuko wa kufa na kuzikana kwa watumishi na kupendekeza kuwa kila Mtumishi kuchangia shilingi elfu mbili kila mwezi ambayo itakatwa kwenye mshahara wake.
Akiwasilisha hoja hiyo kwenye Mkutano wa baraza la wafanyakzi uliofanyika Novemba 10,2021 katika Ukumbi wa Shule ya Sekondari ya Ufundi, Katibu wa baraza la wafanyakazi Manispaa ya Mtwara-Mikindani Justine Mkwara amesema kuwa mfuko huu unaanzishwa ili kuleta usawa kwenye masuala ya kupeana pole pindi mtumishi anapopatwa na msiba na kuondoa utaratibu unaotumika sasa wa kupitisha karatasi ya kuchangia rambirambi kwenye Ofisi.
Ameendelea kusema kuwa mfuko huo utatoa shilingi 500,000 pindi mtumishi atakapofariki au kufiwa na ndugu wa karibu wakiwemo baba, mama, mke, mume pamoja na watoto wanne ambao mtumishi atakuwa amewaandika kwenye orodha ya wategemezi itakayoandaliwa na kwamba fedha zote ziatakazokusanywa zitawekwa kwenye akaunti maalumu na kusimamiwa na Kamati maalumu ya watu wasiozidi watano.
Kwa upande wake Afisa Utumishi wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani Bi. Tamko Ally amesema kuwa uwepo wa mfuko huu haiondoi stahiki kama hizo anazostahili kuzipata mtumishi kutoka kwa mwajiri na kusisitiza kuwa mfuko huo ni wa hiyari hivyo wanufaika ni wale tu ambao watakuwa tayari kukatwa kwenye mshahara kwa kujaza fomu maalumu.
Aidha amewataka wajumbe wa baraza hilo kila mmoja kwa uwakilishi wake akafikishe ujumbe huu kwa watumishi anaowawakilisha ili kila mmoja aweze kuridhia kujiunga na mfuko huu muhimu wa kufa na kuzikana
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.