Ikiwa leo Septemba 24 ni siku ya usafi wa mwisho wa mwezi, Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara-mikindani Col. Emanuel Mwaigobeko ameungana na Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi Kata ya Likombe kufanya usafi katika kituo cha afya cha Likombe na kuwashukuru wanachama hao kwa kujitokeza kwa wingi.
MKurugenzi amewapongeza wanachama hao pia kwa kutoa msaada wa sabuni ya unga ya kufulia itakayosaidia kufanya usafi katika kituo hiko na kutoa wito Kwa Kata zingine kuiga mfano wa Kata ya Likombe ya kujitokeza kufanya usafi kila jumamosi ya mwisho wa mwezi na kutoa misaada ya kijamii.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Kata ya Likombe amesema kuwa wao kama chama wameamua kufanya usafi kwenye eneo la hospitali na kutoa sabuni ili kuweka sehemu hiyo katika hali ya usafi na kuimarisha afya.
Nae Diwani wa Kata ya Likombe Mhe. Saidi Salumu Seiph amewashukuru wananchi wake kwa kujitokeza kufanya usafi na amesema kuwa huo utakuwa utamaduni wao wa kila mwisho wa mwezi kuchagua eneo la kufanya usafi ikiwemo Shule ya sekondari ya mfano ya Likombe.
Aidha Kutokana na uhaba wa vifaa vya usafi katika Kituo hiko Mhe.Diwani amewaomba wana Mtwara na wadau wengine kujitokeza na kuchangia vifaa hivyo.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.