Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Philip Isdor Mpango amewata wafanyabiashara waliokuwa wanafanya biashara Soko la Saba Saba kuhamia soko la Chuno.
"Hii ni kauli ya Serikali ninawasihi wale ambao hawajaenda Soko la Chuno waende msing’ang’anie huko muliko” Amesema Makamu wa Rais
Mhe. Makamu wa Rais amemuagiza Mkuu wa Mkoa na Mkuu wa Wilaya kutenga siku moja kusikiliza kero na malalamiko ya wananchi na kutoa rai kwa wananchi wenye malalamiko kuwasilisha malalamiko yao katika ofisi hizo.
Aidha Makamu wa Rais ameunda timu kutoka TAMISEMI kwa ajili ya kushughulikia malalamiko ya wafanyabiashara waliokuwa Saba Saba kuhusu kubomolewa mabanda yao ya biashara bila kulipwa chochote
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.