Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani COL. Emanuel Mwaigobeko amegawa vishkwambi 482 vilivyotumika kwenye zoezi la sensa ya watu na makazi kwa watumishi wa sekta ya elimu Msingi na Sekondari.
Akikabidhi vishkwambi hivyo Januari 10,2023 katika Ukumbi wa Manispaa kwa Maafisa Elimu COL. Emaneul Mwaigobeko amesema kuwa divisheni ya elimu Misngi itapokea vishkwambi 212 huku divisheni ya Elimu Sekondani ikipokea vishkwambi 270.
COL. Mwaigobeko amewataka walimu wote watakaopata vifaa hivyo kuvitumia kwa matumizi yanayolenga kupandisha kiwango cha elimu na sio matumizi binafi.
Nae Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Rahaleo mwalimu Julius Mkuwele ameishukuru Serikali kwa kujali na kutambua juhudi za walimu katika kukuza elimu yetu.
Amesema kuwa vitendea kazi hivyo vitasaidia kutunza kumbukumbu mbalimbali za shule , kuandaa nukuu za masomo na kupokea taarifa mbalimbali za uongozi wa juu.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.