Aliyekuwa wa Wilaya ya Mtwara Mhe.Mwanahamisi Munkunda amesema kuwa anaondoka Wilaya ya Mtwara akiwa bado anapatamani na kwamba amefurahi Kufanya kazi na wadau mbalimbali Kwa kuwa amepata ujuzi wa Kutosha .
Amesema kuwa anaondoka akiwa na utimamu wa afya kama ambavyo aliahidiwa wakati anafika Mtwara kuiongoza Wilaya hiyo.
Mhe. Munkunda ameyasema hayo Leo Septemba 5,2024 alipokuwa anazungumza na Viongozi na wananchi Kwenye hafla ya kukabidhi Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Kwa Mkuu wa Wilaya hiyo Mpya Mhe.Abdallah Mwaipaya.
Kutokana na uwepo wa vivutio mbalimbali Katika Mkoa wa Mtwara Mhe.Munkunda ameahidi kurudi tena Mtwara Kufanya utalii Kwa kuwa Kuna vivutio vizuri.
Aidha amemshukuru Mkuu wa Mkoa wa Mtwara COL. Patrick Sawala, wananchi,Viongozi na wadau mbalimbali Kwa ushirikiano aliopewa katika kipindi chote cha uongozi wake.
Amechukua Nafasi hiyo kuwaomba Wana Mtwara kumpa ushirikiano Mkuu wa Wilaya Mpya Katika majukumu yake ya Kila siku.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.