Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Abdallah Mwaipaya ameahidi Kufanya kazi na wananchi wa Wilaya ya Mtwara Kwa Unyenyekevu mkubwa na Kwa kufuata misingi mizuri iliyowekwa na Mkuu wa Wilaya aliyepita.
Amesema kuwa atajitahidi kuwafikia wananchi wote na kutatua changamoto zao huku akiomba kupata ushirikiano kutoka kwa wadau wote.
Aidha Kuelekea Uchaguzi Mkuu na Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Mkuu wa Wilaya ameahidi kuandaa tamasha la Uchaguzi "Daftari Festival" ili kutoa elimu Kwa wananchi kuhusu kujiandikisha Kwenye Daftari la kudumu la wapiga kura wakati utakapofika.
Amesema kuwa ni vema wananchi wakajitokeza wakati huo kuboresha taarifa zao ili waweze Kushiriki Kwenye upigaji Kura na Kuchagua Viongozi wanaowataka.
Mkuu wa Wilaya ya Mtwara ameyasema hayo alipozungumza na wananchi na Viongozi mbalimbali Kwenye hafla ya makabidhiano ya Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Leo Septemba 5,2024
Kabla ya kuhamishiwa Wilaya ya Mtwara Mhe. Abdallah Mwaipaya alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Mwanga iliyopo Mkoani Kilimanjaro.
Kwa upande wake Naibu Meya wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani amemkaribisha Mhe.Mwaipaya na kumuahidi kumpatia ushirikiano Kwenye Utekelezaji wa majukumu yake ya kila siku.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.