• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mtwara Mikindani Municipal Council
Mtwara Mikindani Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Manispaa ya Mtwara Mikindani

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Idara
      • Elimu ya Sekondari
      • Elimu ya Msingi
      • Idara ya Maji
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na biashara
      • Afya
      • Usafi na Mazingira
      • Ujenzi
      • Mipango Miji, Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ufugaji na Uvuvi
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
    • Kitengo
      • Ukaguzi wa ndani
      • Teknolojia, Habari, Mawasiliano na Mahusiano
      • Manunuzi na Ugavi
        • Fursa za Uwekezaji
          • Vivutio vya Utalii
          • Maeneo ya Viwanda
      • Ufugaji wa nyuki
      • Uchaguzi
      • Sheria
    • Muundo wa Kiutawala
    • Kata
      • Shangani
      • Rahaleo
      • Reli
      • Vigaeni
      • Majengo
      • Magomeni
      • Ufukoni
      • Mitengo
      • Magengeni
      • Mtonya
      • Kisungule
      • Jangwani
      • Mtawanya
      • Naliendele
      • Chikongola
      • Chuno
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Maeneo ya Viwanda
  • Huduma
    • huduma za maji
    • Huduma za afya
    • Huduma za elimu
    • HUduma za watumishi
    • Uzoaji wa taka ngumu
  • Madiwani
    • Orodha ya Wahe. Wabunge na Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipangomiji na Ujenzi
      • Huduma za Jamii
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Ratiba za Vikao
      • Kumuona Mstahiki Meya
  • Mradi
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi mipya
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Miongozo
    • Fomu
    • Huduma kwa Mteja
    • Ripoti
    • Mpango Mkakati
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Videos
    • Hotuba
    • Maktaba cha Picha

Diwani Mteule wa Kata ya Reli Aapishwa Tayari kwa kuanza Kazi

Posted on: November 30th, 2017

DIWANI MTEULE WA KATA YA RELI AAPISHWA TAYARI KWA KUANZA KAZI.

Diwani mteule wa Kata ya Reli Mh.Genfrid Mbunda  amekula kiapo cha udiwani baaada ya kushinda uchaguzi mdogo wa udiwani katika kata ya Reli uliofanyika Novemba 26 na kupata kura 422 ambayo ni sawa na asilimia 50.96

Akizungumza  Katika hafla fupi ya kuapishwa iliyofanyika kwenye ukumbi wa Manispaa Mtwara-Mikindani Novemba 30 mwaka huu Naibu meya wa Manispaa Mh.Shadida Ndile amemtaka diwani mteule kuwa muadilifu na kushirikiana na Madiwani wenzake pamoja na watendaji ili aweze kufanya kazi vizuri

Aidha Ndile  amesema kuwa kazi nyingi za halmashauri ni za kujitolea hivyo amewaomba  Wananchi wa Reli kumpa ushirikiano wa kutosha diwani wao ili waweze kuleta Maendeleo na  mabadiliko kwenye Kata ya Reli.

Nae Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa Mtwara-Mikindani bi Tamko Ally amempongeza diwani mteule kwa ushindi alioupata na kumkaribisha Manispaa kwa ajili ya kuwatumikia  Wananchi wa Reli kwa kuwa wana imani nae na  wamempa dhamana hiyo.

 Tamko amesema ana imani   kuwa kwa kipindi chote cha uongozi wa diwani huyo  atawatumikia wananchi wake kwa kufuata  sheria, miongoza na kanuzi zote zinazoongoza Manispaa ya Mtwara- Mikindani. Aidha amemkabidhi  vitendea kazi vikiwemo kanuni za kudumu za halmashauri, majukumu ya madiwani, Ratiba ya vikao vya mwaka vya  halmashauri, mipaka ya kijiografia ya manispaa, kitabu cha maadili ya madiwani, ilani ya Chama Cha Mapinduzi na nakala ya kiapo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya Salumu Mhapi amewashukuru wasimamizi wa uchaguzi kwa kuwa wamejitahidi sana kusimamia haki ndio maana uchaguzi  umeisha salama na hakuna vurugu zilizojitokeza.

Akitoa neno la shukrani kwa Wananchi wake Diwani mteule wa Kata hiyo amewaomba ushirikiano wananchi katika utekelezaji wa majukumu yake kwani  yeye peke yake hataweza kufanikiwa.

“Kazi zangu zinatokana na nyinyi nategemea uongozi na ushauri ili niweze kufanya kazi vizuri katika Kata ya Reli na kuleta Maendeleo” alisema Mbunda

Uchaguzi mdogo wa Udiwani nchini umefanyika Novemba 26 mwaka huu na kwa Manispaa ya Mtwara Mikindani vyama vitano vya siasa vimeshiriki uchaguzi huo vikiwemo ACT-Wazalendo, CCM, CHADEMA, CUF na NCCR- MAGEUZI.

 Katika uchaguzi huo Diwani mteule ambae aligombea kwa tiketi ya Chama Chama Mapinduzi amepata kura 422  sawa na asilimia 50.96, akifuatiwa na CHADEMA  kura 356 sawa na asilimia 42.99, ACT- Wazalendo kura 27 sawa na asilimia 3.26, CUF kura 21 sawa na asilimia 2.53 na NCCR Mageuzi kura 2 sawa na asilimia 0.24

Idadi ya wapiga kura waliojiandikisha kwenye daftari la wapiga kura katika Kata ya Reli ni 2320 na idadi ya waliopiga kura ni 842 sawa na asilimia 36.29

Matangazo

  • Taarifa Kwa Umma ya Ilani ya Kuondoka Kwenye Kiwanja Nmaba 1-149 Litingi January 03, 2025
  • Taarifa Kwa Umma Ufafanuzi Kuhusu Jina la Shule ya Sekondari Mwalimu Nyange January 02, 2025
  • Terms Of Reference For The Provisions Of Construction Supervision Consultancy Services For Urban Infrastructures Development In Mtwara Mikindani Municipality Under The TACTIC Project March 07, 2025
  • Tangazo la Kuitwa Kwenye Usaili Nafasi ya Mwandikishaji Msaidizi na BVR Operators January 09, 2025
  • Tazama yote

Habari mpya

  • Kamati ya Siasa Mkoa Yapongeza Utekeelzaji wa Miradi ya MaendeleoMtwara-Mikindani

    January 08, 2025
  • MD Nyange Ateta na Watumishi Wa Kada ya Afya

    January 07, 2025
  • Vikundi Vilivyopata Mkopo Vyahimizwa Kurejesha Fedha Kwa Wakati

    January 06, 2025
  • Mtwara-Mikindani Yatoa Mkopo wa Mil.640.9 Kwa Vikundi 58

    January 06, 2025
  • Tazama yote

Video

Namna ya Kujisajili na Kutumia mfumo wa Uhamisho kwa watumishi wa Umma
Video nyinginezo

Viunganishi vya haraka

  • Zabuni ya ujenzi wa barabara km 4.1,Ujenzi wa Mfereji wa maji ya mvua toka Skoya,nabwada hadi Mtepwezi,Ujenzi wa soko la Chuno,Ukarabati wa stendi ya Mikindani pamoja na Uboreshaji wa sehemu za kupumzikia na michezo
  • Kupata matokeo ya Darasa la nne 2017 Manispaa Mtwara-Mikindani
  • Matokeo ya Kidato cha Pili 2017 Manispaa Mtwara-Mikindani
  • Taratibu za Kupata fomu za Vileo

Viunganishi linganifu

  • Tovuti kuu ya Serikali
  • OR - TAMISEMI
  • Wakala ya Serikali Mtandao
  • Utumishi wa Umma
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Takwimu ya Taifa

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    Manispaa Mtwara-Mikindani

    Anuani ya Posta: P. o. Box 92,

    Simu ya mezani: 023-2333102

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.