• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mtwara Mikindani Municipal Council
Mtwara Mikindani Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Manispaa ya Mtwara Mikindani

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Idara
      • Elimu ya Sekondari
      • Elimu ya Msingi
      • Idara ya Maji
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na biashara
      • Afya
      • Usafi na Mazingira
      • Ujenzi
      • Mipango Miji, Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ufugaji na Uvuvi
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
    • Kitengo
      • Ukaguzi wa ndani
      • Teknolojia, Habari, Mawasiliano na Mahusiano
      • Manunuzi na Ugavi
        • Fursa za Uwekezaji
          • Vivutio vya Utalii
          • Maeneo ya Viwanda
      • Ufugaji wa nyuki
      • Uchaguzi
      • Sheria
    • Muundo wa Kiutawala
    • Kata
      • Shangani
      • Rahaleo
      • Reli
      • Vigaeni
      • Majengo
      • Magomeni
      • Ufukoni
      • Mitengo
      • Magengeni
      • Mtonya
      • Kisungule
      • Jangwani
      • Mtawanya
      • Naliendele
      • Chikongola
      • Chuno
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Maeneo ya Viwanda
  • Huduma
    • huduma za maji
    • Huduma za afya
    • Huduma za elimu
    • HUduma za watumishi
    • Uzoaji wa taka ngumu
  • Madiwani
    • Orodha ya Wahe. Wabunge na Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipangomiji na Ujenzi
      • Huduma za Jamii
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Ratiba za Vikao
      • Kumuona Mstahiki Meya
  • Mradi
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi mipya
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Miongozo
    • Fomu
    • Huduma kwa Mteja
    • Ripoti
    • Mpango Mkakati
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Videos
    • Hotuba
    • Maktaba cha Picha

Madiwani Manispaa Ya Mtwara Wachagua Naibu Meya

Posted on: July 27th, 2017

Madiwani Manispaa ya Mtwara Wachagua Naibu Meya

Baraza la Madiwani la halmashauri ya Manispaa Mtwara-Mikindani limefanya uchaguzi wa Naibu Meya pamoja na uundaji wa kamati za kudumu za halmashauri.

Uchaguzi huo unafanyika kila mwaka kwa kuwa ni matakwa ya kisheria ambapo kila ifikapo mwisho wa mwaka baraza linatakiwa kuchagua Naibu Meya pamoja na   uundaji wa kamati za kudumu. kanuni za kudumu za halmashauri kifungu namba 7(3)kinatoa ufafanuiz wa mchakato mzima wa uchaguzi huo.

Awali akizungumza kwenye baraza hilo kabla ya uchaguzi kuanza, Msimamizi wa uchaguzi ambae pia ni Mkurugenzi wa Manispaa Mtwara Mikindani bi Beatrice Dominic alisema kuwa amepokea majina 3 ya wagombea wa nafasi ya Naibu meya kutoka katika vyama vya CUF, CHADEMA na CCM.

Aliendelea kusema kuwa wajumbe wanaotakiwa kupiga kura kwenye baraza hilo wako 26 na kuwataka wajumbe wao kuzingatia kanuni na tararibu zote za uchaguzi ikiwemo kutobeba simu unapoenda kupiga kura na kuwasisitiza kuwa kura hizo ni za siri hivyo kila mmoja atachagua mgombea anayemtaka kwa siri.

Hata hivyo kabla ya zoezi la upigaji kura halijaanza  wagombea wote walipewa nafasi ya kujieleza,kujinadi pamoja na kuomba kura kwa wajumbe wa baraza. Aidha wapiga kura nao walipata nafasi   ya kuuliza maswali  kwa wagombea.

Aidha Baada ya kukamilika kwa zoezi la upigaji wa kura  msimamizi wa uchaguzi alitangaza matokeo ya uchaguzi huo na kumtangaza  Mhe Shadida Ndile kuwa Naibu meya mpya wa Manispaa Mtwara-Mikindani kwa  kuwa aliongoza kwa kupata kura nyingi kuliko wagombea wengine.

Mhe Shadida ndile  aliongoza kwa kupata kura 14 sawa na asilimia 53, nafasi ya pili imeshikwa na Mhe  Selemani I. Mshamu amepata kura 7 sawa na aslimia 26 na nafasi ya tatu imeshikwa na Mh Erick Mkapa kwa kupata 5 kura ambayo ni sawa na asilimaia 19.

Akitoa neno la shukrani Naibu Meya Wa Manispaa mpya  Mhe Shadida Ndile alisema kuwa anawashukuru wajumbe wote kwa kumchagua wameonesha wana imani na yeye,aidha ameahidi kufanya kazi kwa kushirikiana na kushikama ili kuongeza kasi ya Maendeleo. Ameahidi pia kufanya kazi na Madiwani wote bila ya kujali itikadi ya chama wala siasa.

Nae Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe Evod Mmnda amewapongeza Wajumbe wa baraza hilo kwa kuonesha ukomavu wa kisiasa kwani uchaguzi umeanza vizuri na umeisha vizuri bila ya vurugu zozote kama sehemu nyingine zinavyokuwa. Aidha amewataka Madiwani na watendaji kufanya kazi kwa kushirikiana kwa Maendeleo ya wana Mtwara.

Kwa upande wake Mstahiki Meya wa Halmashauri amempongeza Mh Shadida kwa kupata ushindi na kwamba ana imani watafanya kazi pamoja na kwa kushirikiana. Amesisitiza kuwa yeye kama meya wa halmashauri ataendelea kuisimamia na kuitekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi kwani ndio chama ambacho kipo madarakani.

Kamati za kudumu za halamashauri zilizoundwa ni pamoja na Kamati ya Huduma za Jamii inayoongozwa na Mhe Hassan Namkami pamoja na Kamati ya Mipango Miji na Mazingira inayoongozwa na Mhe Yakuti T Yakuti.

Matangazo

  • Taarifa Kwa Umma ya Ilani ya Kuondoka Kwenye Kiwanja Nmaba 1-149 Litingi January 03, 2025
  • Taarifa Kwa Umma Ufafanuzi Kuhusu Jina la Shule ya Sekondari Mwalimu Nyange January 02, 2025
  • Terms Of Reference For The Provisions Of Construction Supervision Consultancy Services For Urban Infrastructures Development In Mtwara Mikindani Municipality Under The TACTIC Project March 07, 2025
  • Tangazo la Kuitwa Kwenye Usaili Nafasi ya Mwandikishaji Msaidizi na BVR Operators January 09, 2025
  • Tazama yote

Habari mpya

  • Kamati ya Siasa Mkoa Yapongeza Utekeelzaji wa Miradi ya MaendeleoMtwara-Mikindani

    January 08, 2025
  • MD Nyange Ateta na Watumishi Wa Kada ya Afya

    January 07, 2025
  • Vikundi Vilivyopata Mkopo Vyahimizwa Kurejesha Fedha Kwa Wakati

    January 06, 2025
  • Mtwara-Mikindani Yatoa Mkopo wa Mil.640.9 Kwa Vikundi 58

    January 06, 2025
  • Tazama yote

Video

Namna ya Kujisajili na Kutumia mfumo wa Uhamisho kwa watumishi wa Umma
Video nyinginezo

Viunganishi vya haraka

  • Zabuni ya ujenzi wa barabara km 4.1,Ujenzi wa Mfereji wa maji ya mvua toka Skoya,nabwada hadi Mtepwezi,Ujenzi wa soko la Chuno,Ukarabati wa stendi ya Mikindani pamoja na Uboreshaji wa sehemu za kupumzikia na michezo
  • Kupata matokeo ya Darasa la nne 2017 Manispaa Mtwara-Mikindani
  • Matokeo ya Kidato cha Pili 2017 Manispaa Mtwara-Mikindani
  • Taratibu za Kupata fomu za Vileo

Viunganishi linganifu

  • Tovuti kuu ya Serikali
  • OR - TAMISEMI
  • Wakala ya Serikali Mtandao
  • Utumishi wa Umma
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Takwimu ya Taifa

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    Manispaa Mtwara-Mikindani

    Anuani ya Posta: P. o. Box 92,

    Simu ya mezani: 023-2333102

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.