Waheshimiwa Madiwani toka Halmashauri ya wilaya ya Mkuranga wameipongeza Halmashauri ya Manispaa Mtwara-Mikindani kwa mikakati na mipango yake kabambe katika kukusanya mapato ya Uvuvi na Ushuru mwingine.
Wakiongea wakati wa ziara yao ya kujifunza katika Manispaa ya Mtwara-Mikindani, Madiwani hao wamesema wameridhishwa na repoti zilizowasilishwa na Idara ya Uvuvi, Idara ya Mipangomiji pamoja na mikakati ya ukusanyaji mapato yatokanayo na zao la Korosho.
Madiwani hao wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mkuranga, Mhe. Mohamed Maundu, leo tarehe 29, Oktoba, 2024 wamefanya ziara hiyo ya kujifunza, ambapo wametembelea maeneo mbalimbali ikiwemo soko la samaki Feri, vizimba vya kufugia majongoo bahari na mengi
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.