• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mtwara Mikindani Municipal Council
Mtwara Mikindani Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Manispaa ya Mtwara Mikindani

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Idara
      • Elimu ya Sekondari
      • Elimu ya Msingi
      • Idara ya Maji
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na biashara
      • Afya
      • Usafi na Mazingira
      • Ujenzi
      • Mipango Miji, Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ufugaji na Uvuvi
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
    • Kitengo
      • Ukaguzi wa ndani
      • Teknolojia, Habari, Mawasiliano na Mahusiano
      • Manunuzi na Ugavi
        • Fursa za Uwekezaji
          • Vivutio vya Utalii
          • Maeneo ya Viwanda
      • Ufugaji wa nyuki
      • Uchaguzi
      • Sheria
    • Muundo wa Kiutawala
    • Kata
      • Shangani
      • Rahaleo
      • Reli
      • Vigaeni
      • Majengo
      • Magomeni
      • Ufukoni
      • Mitengo
      • Magengeni
      • Mtonya
      • Kisungule
      • Jangwani
      • Mtawanya
      • Naliendele
      • Chikongola
      • Chuno
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Maeneo ya Viwanda
  • Huduma
    • huduma za maji
    • Huduma za afya
    • Huduma za elimu
    • HUduma za watumishi
    • Uzoaji wa taka ngumu
  • Madiwani
    • Orodha ya Wahe. Wabunge na Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipangomiji na Ujenzi
      • Huduma za Jamii
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Ratiba za Vikao
      • Kumuona Mstahiki Meya
  • Mradi
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi mipya
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Miongozo
    • Fomu
    • Huduma kwa Mteja
    • Ripoti
    • Mpango Mkakati
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Videos
    • Hotuba
    • Maktaba cha Picha

Mil. 14.9 za Mfuko wa Elimu Mtwara-Mikindani Kukarabati Vyoo,Madarasa

Posted on: July 1st, 2020

Baada ya kufanya kazi kubwa ya kuhamasisha jamii juu ya uchangiaji katika sekta ya elimu na kukusanya fedha  kupitia mfuko wa elimu wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani, Bodi ya mfuko wa Elimu ya Manispaa imefanikiwa kukusanya shilingi 14,978,270 na kuzipeleka katika shule za Msingi na Sekondari kwa ajili ya kukarabati miundombinuya vyoo na madarasa.

Akizungumza wakati wa kukabidhi hundi kwa shule hizo Julai 1,2020 Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Dunstan Kyobya ameipongeza bodi hiyo kwa kazi kubwa waliyoifanya ya kuhamasisha  na kufanikiwa   kukusanya kiasi hiko cha fedha kitakachotumika kukarabati baadhi ya majengo katika Shule.

Pamoja na pongezi hizo Kyobya ameitaka bodi hiyo kuhakikisha inatembelea shule zote zilizopata fedha ili kujua kama zimetumika kama ilivyokusudiwa  lakini pia kujua changamoto zilizopo pamoja na mahitaji mengine.

Aidha ametoa siku kumi na sita kwa shule zilizopata fedha kuhakikisha wanakamilisha ukarabati wa miundombinu hiyo na kuwataka walimu wakuu na watendaji wa Kata kuhakikisha kuwa Kampeni ya  Shule ni Choo iliyoanzishwa na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Gelasius Byakanwa inasimamiwa vizuri.

Awali akisoma taarifa ya Mfuko wa Elimu wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Elimu Bwana. Symthies Pangisa amesema kuwa kwa mwaka wa fedha wa 2019/2020 Bodi hiyo imekusanya shilingi 14,978,270 kati ya 396,008,000 zilizotarajiwa kukusanywa kutoka kwa jamii.

Amesema kuwa kiasi cha fedha kilichokusanywa kimegawiwa kwa baadhi ya Shule za Msingi za Chuno, Misufini na  Sekondari ya SabaSaba na Mitengo  kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa matundu ya vyoo  Pamoja na kukarabati miundombinu iliyochakaa ya Shule ya Sekondari ya Umoja.

Pangisa amezitaja changamoto mbalimbali zilizopo katika jamii zilizopelekea kukusanya kiasi kidogo cha fedha ikiwemo uelewa mdogo wa wananchi katika kuchangia Elimu, ugumu wa wnaanchi kuchangia katika elimu Pamoja na uelewa mdogo kwa wasimamizi na wakusanyaji wa michango ya mfuko wa Elimu.

Kwa upande wake Afisa Mtendaji wa Kata ya Chuno Bi. Hadija Mkongo ameishukuru bodi kwa fedha hizo na kuahidi kuendelea kuhamasisha na kukusanya fedha za mfuko wa Elimu na kuifanya ajenda ya kudumu kwenye vikao vya Kata.

Mfuko wa Elimu wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani umeundwa chini ya jedwali la kwanza la sharia ndogo ya Uanzishwaji wa bodi ya mfuko wa elimu  za halmashauri ya Manispaa ya Mtwara-Mikindani za mwaka 2004 katika  tangazo la Serikali na 360 la mwaka 2014. Aidha Bodi yaMfuko wa Elimu  iliundwa mwishoni mwa mwaka 2017 kwa lengo la kutoa hamasa ya uchangiaji wa mfuko wa kwa jamii,

Matangazo

  • Taarifa Kwa Umma ya Ilani ya Kuondoka Kwenye Kiwanja Nmaba 1-149 Litingi January 03, 2025
  • Taarifa Kwa Umma Ufafanuzi Kuhusu Jina la Shule ya Sekondari Mwalimu Nyange January 02, 2025
  • Terms Of Reference For The Provisions Of Construction Supervision Consultancy Services For Urban Infrastructures Development In Mtwara Mikindani Municipality Under The TACTIC Project March 07, 2025
  • Tangazo la Kuitwa Kwenye Usaili Nafasi ya Mwandikishaji Msaidizi na BVR Operators January 09, 2025
  • Tazama yote

Habari mpya

  • Kamati ya Siasa Mkoa Yapongeza Utekeelzaji wa Miradi ya MaendeleoMtwara-Mikindani

    January 08, 2025
  • MD Nyange Ateta na Watumishi Wa Kada ya Afya

    January 07, 2025
  • Vikundi Vilivyopata Mkopo Vyahimizwa Kurejesha Fedha Kwa Wakati

    January 06, 2025
  • Mtwara-Mikindani Yatoa Mkopo wa Mil.640.9 Kwa Vikundi 58

    January 06, 2025
  • Tazama yote

Video

Namna ya Kujisajili na Kutumia mfumo wa Uhamisho kwa watumishi wa Umma
Video nyinginezo

Viunganishi vya haraka

  • Zabuni ya ujenzi wa barabara km 4.1,Ujenzi wa Mfereji wa maji ya mvua toka Skoya,nabwada hadi Mtepwezi,Ujenzi wa soko la Chuno,Ukarabati wa stendi ya Mikindani pamoja na Uboreshaji wa sehemu za kupumzikia na michezo
  • Kupata matokeo ya Darasa la nne 2017 Manispaa Mtwara-Mikindani
  • Matokeo ya Kidato cha Pili 2017 Manispaa Mtwara-Mikindani
  • Taratibu za Kupata fomu za Vileo

Viunganishi linganifu

  • Tovuti kuu ya Serikali
  • OR - TAMISEMI
  • Wakala ya Serikali Mtandao
  • Utumishi wa Umma
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Takwimu ya Taifa

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    Manispaa Mtwara-Mikindani

    Anuani ya Posta: P. o. Box 92,

    Simu ya mezani: 023-2333102

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.