• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mtwara Mikindani Municipal Council
Mtwara Mikindani Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Manispaa ya Mtwara Mikindani

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Idara
      • Elimu ya Sekondari
      • Elimu ya Msingi
      • Idara ya Maji
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na biashara
      • Afya
      • Usafi na Mazingira
      • Ujenzi
      • Mipango Miji, Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ufugaji na Uvuvi
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
    • Kitengo
      • Ukaguzi wa ndani
      • Teknolojia, Habari, Mawasiliano na Mahusiano
      • Manunuzi na Ugavi
        • Fursa za Uwekezaji
          • Vivutio vya Utalii
          • Maeneo ya Viwanda
      • Ufugaji wa nyuki
      • Uchaguzi
      • Sheria
    • Muundo wa Kiutawala
    • Kata
      • Shangani
      • Rahaleo
      • Reli
      • Vigaeni
      • Majengo
      • Magomeni
      • Ufukoni
      • Mitengo
      • Magengeni
      • Mtonya
      • Kisungule
      • Jangwani
      • Mtawanya
      • Naliendele
      • Chikongola
      • Chuno
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Maeneo ya Viwanda
  • Huduma
    • huduma za maji
    • Huduma za afya
    • Huduma za elimu
    • HUduma za watumishi
    • Uzoaji wa taka ngumu
  • Madiwani
    • Orodha ya Wahe. Wabunge na Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipangomiji na Ujenzi
      • Huduma za Jamii
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Ratiba za Vikao
      • Kumuona Mstahiki Meya
  • Mradi
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi mipya
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Miongozo
    • Fomu
    • Huduma kwa Mteja
    • Ripoti
    • Mpango Mkakati
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Videos
    • Hotuba
    • Maktaba cha Picha

Milioni 257.1 zawanufaisha Wanawake, Vijana na Walemavu Mtwara-Mikindani

Posted on: June 12th, 2020




Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Dunstan Kyobya  akikabidhi bodaboda sita kwa vikundi viwili vya vijana vya Umoja na Kijana Jitume (Kata ya Shangani) ikiwa ni sehemu ya mkopo walipatiwa kutoka kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani.

Katika kuhakikisha kuwa wananchi wanawezeshwa kiuchumi ili waweze kujiongezea kipato na kujikimu kimaisha Manispaa ya Mtwara-Mikindani kupitia mapato yake ya ndani imetoa mkopo wa shilingi Milioni 257.1 kwa vikundi 56 vya wajasiriamali wakiwemo  wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.

Akizungumza kwenye hafla fupi ya kukabidhi hundi ya mkopo kwa vikundi hivyo iliyofanyika Juni 12,2020 katika viwanja vya Ofisi za Manispaa, Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Dunstan Kyobya amempongeza Mkurugenzi kwa kutii agizo la Serikali la kutenga asilimia 10 ya mapato ya ndani kwa ajili ya kuwakopesha wajasiriamali.

Pamoja na pongezi hizo Kyobya pia amevitaka vikundi vilivyopatiwa mkopo kutumia fedha hizo kwa matumizi yaliyokusudiwa ili waweze kurejesha fedha kwa wakati na wengine waweze kunufaika.

“Hii sio pesa ya kwenda kununua nguo, hii sio pesa ya kwenda kununua nyumba, huu ni mkopo unaosaidia kujikwamua kimaisha ,ukikopa lazima ulipe kwa wakati”alisema Kyobya

Kyobya pia amesisitiza kupelekewa mahakamani kwa wale wote watakaoshindwa kurejesha mikopo na kuwataka vijana kukaza buti ili waweze kurejesha mkopo waliopewa.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara-Miindani Col. Emanuel Mwaigobeko amesema kuwa ana Imani mkopo uliotolewa kwa wajasiriamali haoutawasaidia ,kujiajiri Pamoja na kuyafanya Maisha yao kuwa bora.

Awali akisoma taarifa ya utoaji wa mikopo Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya jamii Bi Juliana Manyama amesema kuwa mkopo umetolewa  kwa vikundi vya wanawake 42 vyenye mkopo wa wa shilingi 175,100,000, watu wenye ulemavu vikundi 3 vyenye mkopo wa shilingi 7,500,000 na Vijana vikundi 11 vilivyopata mkopo wa shilingi 74,500,000  na bodaboda 6 na kufanya idadi ya vikundi  vilivyopata mkopo kuwa 56.

Ameongeza kuwa Katika mwaka wa fedha wa 2019/2020 Manispaa ya Mtwara-Mikindani imekopesha shilingi 447,100,000 kwa vikundi 80 vya wajasiriamali vikiwemo vikundi vya wanawake 47, Vijana 27 na watu wenye ulemavu vikundi 6.

Pamoja na fedha zilizokopeshwa pia katika bajeti yake ya 2019/2020 halmashauri imepekea kwenye mfuko wa wanawake, Vijana na walemavu shilingi Milioni 339,000,000 sawa na asilimia 100 ya kiasi kinachotakiwa kuchangia katika mfuko mfuko wa vikundi.

Wakati huo huo Saidi Chinamenga Mjasiriamali wa kuuza genge amepokea kwa furaha mkopo huo na kuishukuruSerikali ya awamu ya tano kwa kuwaenzi walemavu na ameahidi kufanya kaiz kwa bidi ili aweze kurejesha mkopo kwa wakati.

Nae Podensiana Sungura mfugaji wa kuku amesema kuwa mkopo walioupata utasaidia kukuza mtaji wao na kuweza kulea familia zao na ameaasa waliochukua mkopo kurejesha kwa wakati.

Matangazo

  • Taarifa Kwa Umma ya Ilani ya Kuondoka Kwenye Kiwanja Nmaba 1-149 Litingi January 03, 2025
  • Taarifa Kwa Umma Ufafanuzi Kuhusu Jina la Shule ya Sekondari Mwalimu Nyange January 02, 2025
  • Terms Of Reference For The Provisions Of Construction Supervision Consultancy Services For Urban Infrastructures Development In Mtwara Mikindani Municipality Under The TACTIC Project March 07, 2025
  • Tangazo la Kuitwa Kwenye Usaili Nafasi ya Mwandikishaji Msaidizi na BVR Operators January 09, 2025
  • Tazama yote

Habari mpya

  • Kamati ya Siasa Mkoa Yapongeza Utekeelzaji wa Miradi ya MaendeleoMtwara-Mikindani

    January 08, 2025
  • MD Nyange Ateta na Watumishi Wa Kada ya Afya

    January 07, 2025
  • Vikundi Vilivyopata Mkopo Vyahimizwa Kurejesha Fedha Kwa Wakati

    January 06, 2025
  • Mtwara-Mikindani Yatoa Mkopo wa Mil.640.9 Kwa Vikundi 58

    January 06, 2025
  • Tazama yote

Video

Namna ya Kujisajili na Kutumia mfumo wa Uhamisho kwa watumishi wa Umma
Video nyinginezo

Viunganishi vya haraka

  • Zabuni ya ujenzi wa barabara km 4.1,Ujenzi wa Mfereji wa maji ya mvua toka Skoya,nabwada hadi Mtepwezi,Ujenzi wa soko la Chuno,Ukarabati wa stendi ya Mikindani pamoja na Uboreshaji wa sehemu za kupumzikia na michezo
  • Kupata matokeo ya Darasa la nne 2017 Manispaa Mtwara-Mikindani
  • Matokeo ya Kidato cha Pili 2017 Manispaa Mtwara-Mikindani
  • Taratibu za Kupata fomu za Vileo

Viunganishi linganifu

  • Tovuti kuu ya Serikali
  • OR - TAMISEMI
  • Wakala ya Serikali Mtandao
  • Utumishi wa Umma
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Takwimu ya Taifa

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    Manispaa Mtwara-Mikindani

    Anuani ya Posta: P. o. Box 92,

    Simu ya mezani: 023-2333102

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.