• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mtwara Mikindani Municipal Council
Mtwara Mikindani Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Manispaa ya Mtwara Mikindani

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Idara
      • Elimu ya Sekondari
      • Elimu ya Msingi
      • Idara ya Maji
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na biashara
      • Afya
      • Usafi na Mazingira
      • Ujenzi
      • Mipango Miji, Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ufugaji na Uvuvi
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
    • Kitengo
      • Ukaguzi wa ndani
      • Teknolojia, Habari, Mawasiliano na Mahusiano
      • Manunuzi na Ugavi
        • Fursa za Uwekezaji
          • Vivutio vya Utalii
          • Maeneo ya Viwanda
      • Ufugaji wa nyuki
      • Uchaguzi
      • Sheria
    • Muundo wa Kiutawala
    • Kata
      • Shangani
      • Rahaleo
      • Reli
      • Vigaeni
      • Majengo
      • Magomeni
      • Ufukoni
      • Mitengo
      • Magengeni
      • Mtonya
      • Kisungule
      • Jangwani
      • Mtawanya
      • Naliendele
      • Chikongola
      • Chuno
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Maeneo ya Viwanda
  • Huduma
    • huduma za maji
    • Huduma za afya
    • Huduma za elimu
    • HUduma za watumishi
    • Uzoaji wa taka ngumu
  • Madiwani
    • Orodha ya Wahe. Wabunge na Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipangomiji na Ujenzi
      • Huduma za Jamii
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Ratiba za Vikao
      • Kumuona Mstahiki Meya
  • Mradi
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi mipya
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Miongozo
    • Fomu
    • Huduma kwa Mteja
    • Ripoti
    • Mpango Mkakati
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Videos
    • Hotuba
    • Maktaba cha Picha

"Natoa Miezi Mitatu Kila mmoja awe amejiandikisha kwenye Daftari la Wakazi" RC BYAKANWA

Posted on: January 20th, 2018

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe: Gelasius G. Byakanwa akizindua zoezi la Uandikishaji Daftari la Wakazi Kimkoa lililofanyika kwenye Viwanja vya Ofisi  ya Kata Shangani

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe: Gelasius Byakanwa ametoa muda wa miezi mitatu kwa wakazi wa Mkoa wa Mtwara  kujiandikisha  kwenye daftari la wakazi lililopo kwenye kila Mtaa.

Amesema kuwa kama muda huo utapita na mwananchi hajajiandikisha  kwenye daftari hilo  hatatoa adhabu yeyote, badala yake mwananchi atakosa huduma mbalimbali kutoka kwenye Ofisi za Serikali ikiwemo barua za utambulisho zinazotakiwa kwenye mabenki na huduma zingine..

Byakanwa amezungumza hayo leo wakati wa uzinduzi wa zoezi la Uandikishaji kwenye daftari la wakazi Kimkoa  lililofanyika kwenye Viwanja vya Ofisi ya Kata Shangani  Manispaa Mtwara-Mikindani. Aidha amewataka watendaji kutomkaribisha mgeni yeyote kwenye Mtaa kama hana taarifa za kujiandikisha kwenye mtaa alikotokea.

Amesitiza kuwa ili kuendelea kulinda amanii, utulivu  na kuondoa uhalifu  kwenye maeneo yao ni lazima wananchi wakafahamiana kwa kujiandikisha kwenye daftari la wakazi linalomilikiwa na Mtendaji wa Mtaa. Pia ameagiza mtu yeyote anapohamia kwenye  mtaa ni lazima ajiandikishe kwenye daftari hilo ili taarifa zake zingizwe.

Mkuu huyo wa Mkoa amezitaja faida zitokanazo na wananchi kujiandikisha kwenye daftari la wakazi  kuwa ni pamoja na kusaidia Serikali  kupanga bajeti ,mahitaji ,na huduma za jamii kwa watu wake kwa kuwa takwimu za idadi ya watu waliopo kwenye mitaa, kata, tarafa, wilaya, mkoa hadi Taifa  zitakuwepo. Faida zingine ni pamoja na kuimarisha Ulinzi na Usalama.


Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa Mtwara-Mikindani Bi Beatrice Dominic amesema kuwa kutokana na uelewa mdogo wa wananchi juu ya zoezi hili, imepelekea idadi ya waliosajiliwa  kwenye daftari la wakazi kwa Manispaa kuwa ndogo na kufikia watu  46,704 Kati ya Wakazi 115,114 wanaokadiriwa kuwepo kwenye Manispaa. Aidha amesema kuwa anatarajia  baada ya uzinduzi huo wananchi watatimiza wajibu wao kwa kujiandikisha kwenye daftari hilo.

Ameongeza kuwa Daftari hilo litatunzwa na Mwenyekiti wa Mtaa husika na kwamba Mwenyekiti atapaswa kujaza fomu kila  taarifa mpya zinapojitokeza zikiwemo vizazi,Vifo, kuhama na kuhamia. Aidha kazi za Mtendaji wa Mtaa ni kuhakikisha daftari linaingizwa Taarifa, linatunzwa na linatumika.

Daftari la wakazi lipo kisheria chini ya  sheria ya Serikali za Mitaa Na. 6  ya mwaka 1982, na limechapishwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI mwaka 2011.


Matangazo

  • Taarifa Kwa Umma ya Ilani ya Kuondoka Kwenye Kiwanja Nmaba 1-149 Litingi January 03, 2025
  • Taarifa Kwa Umma Ufafanuzi Kuhusu Jina la Shule ya Sekondari Mwalimu Nyange January 02, 2025
  • Terms Of Reference For The Provisions Of Construction Supervision Consultancy Services For Urban Infrastructures Development In Mtwara Mikindani Municipality Under The TACTIC Project March 07, 2025
  • Tangazo la Kuitwa Kwenye Usaili Nafasi ya Mwandikishaji Msaidizi na BVR Operators January 09, 2025
  • Tazama yote

Habari mpya

  • Kamati ya Siasa Mkoa Yapongeza Utekeelzaji wa Miradi ya MaendeleoMtwara-Mikindani

    January 08, 2025
  • MD Nyange Ateta na Watumishi Wa Kada ya Afya

    January 07, 2025
  • Vikundi Vilivyopata Mkopo Vyahimizwa Kurejesha Fedha Kwa Wakati

    January 06, 2025
  • Mtwara-Mikindani Yatoa Mkopo wa Mil.640.9 Kwa Vikundi 58

    January 06, 2025
  • Tazama yote

Video

Namna ya Kujisajili na Kutumia mfumo wa Uhamisho kwa watumishi wa Umma
Video nyinginezo

Viunganishi vya haraka

  • Zabuni ya ujenzi wa barabara km 4.1,Ujenzi wa Mfereji wa maji ya mvua toka Skoya,nabwada hadi Mtepwezi,Ujenzi wa soko la Chuno,Ukarabati wa stendi ya Mikindani pamoja na Uboreshaji wa sehemu za kupumzikia na michezo
  • Kupata matokeo ya Darasa la nne 2017 Manispaa Mtwara-Mikindani
  • Matokeo ya Kidato cha Pili 2017 Manispaa Mtwara-Mikindani
  • Taratibu za Kupata fomu za Vileo

Viunganishi linganifu

  • Tovuti kuu ya Serikali
  • OR - TAMISEMI
  • Wakala ya Serikali Mtandao
  • Utumishi wa Umma
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Takwimu ya Taifa

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    Manispaa Mtwara-Mikindani

    Anuani ya Posta: P. o. Box 92,

    Simu ya mezani: 023-2333102

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.