• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mtwara Mikindani Municipal Council
Mtwara Mikindani Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Manispaa ya Mtwara Mikindani

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Idara
      • Elimu ya Sekondari
      • Elimu ya Msingi
      • Idara ya Maji
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na biashara
      • Afya
      • Usafi na Mazingira
      • Ujenzi
      • Mipango Miji, Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ufugaji na Uvuvi
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
    • Kitengo
      • Ukaguzi wa ndani
      • Teknolojia, Habari, Mawasiliano na Mahusiano
      • Manunuzi na Ugavi
        • Fursa za Uwekezaji
          • Vivutio vya Utalii
          • Maeneo ya Viwanda
      • Ufugaji wa nyuki
      • Uchaguzi
      • Sheria
    • Muundo wa Kiutawala
    • Kata
      • Shangani
      • Rahaleo
      • Reli
      • Vigaeni
      • Majengo
      • Magomeni
      • Ufukoni
      • Mitengo
      • Magengeni
      • Mtonya
      • Kisungule
      • Jangwani
      • Mtawanya
      • Naliendele
      • Chikongola
      • Chuno
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Maeneo ya Viwanda
  • Huduma
    • huduma za maji
    • Huduma za afya
    • Huduma za elimu
    • HUduma za watumishi
    • Uzoaji wa taka ngumu
  • Madiwani
    • Orodha ya Wahe. Wabunge na Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipangomiji na Ujenzi
      • Huduma za Jamii
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Ratiba za Vikao
      • Kumuona Mstahiki Meya
  • Mradi
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi mipya
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Miongozo
    • Fomu
    • Huduma kwa Mteja
    • Ripoti
    • Mpango Mkakati
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Videos
    • Hotuba
    • Maktaba cha Picha

TASAF Yakabidhi Ruzuku Ya Mil.1.8 Kwa Vikundi Vya Kuwekeza na Kuweka Akiba

Posted on: December 2nd, 2017

TASAF Yakabidhi Ruzuku  Ya  Mil.1.8 Kwa  Vikundi Vya   Kuwekeza na  Kuweka Akiba

Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Ladislaus Mwamanga amekabidhi fedha taslimu shilingi milioni 1.800,000 kwa vikundi sita vya kuweka akiba na kuwekeza vilivyopo kwenye mpango wa kunusuru kaya masikini waliopo  mtaa wa Chipuputa.

Fedha zilizotolewa ilikuwa ni kutimiza ahadi waliyowaahidi wana vikundi hao baada ya kuwatembelea septemba mwaka jana na kukuta walengwa hao tayari wameshaanza kuweka akiba na kuwekeza kabla mpango huo haujaanzishwa na TASAF.

Akizungumza kwenye mkutano wa kukabidhi fedha hizo uliofanyika Disemba 1 mwaka huu kwenye kiwanja cha mikutano  Chipuputa Mwamanga amesema kuwa kutokana na ubunifu waliouonesha wanavikundi  hao wa kuuziana sabuni, sukari na vitu vingine waliona ni vema wawaongezee nguvu  kwa kuwapa ruzuku itakayoongeza mtaji kwenye mfuko wao wa kuweka akiba na kukopeshana.

Mwamanga amesema kuwa fedha hizo hazina masharti hivyo walengwa waziingize kwenye utaratibu wao wa siku zote kwa kuwa TASAF ina heshimu sana ushirikishwaji wa jamii na mawazo ya Wananchi. Aidha amesema lengo la kuwaongezea fedha hizo ni kuimarisha vikundi na kuwahamasisha watu wajishughulishe ili waweze kuzalisha na kusonga mbele.

Ameongeza kuwa utoaji wa ruzuku haujaishia kwenye vikundi hivyo tayari TASAF imeshakamilisha muundo ambao utashindanisha vikundi vinavyoweka akiba na kuwekeza na kikundi kitakachofanya vizuri kitaongezewa ruzuku ili viendelee kuwa vizuri zaidi.

Amesema kuwa hadi sasa TASAF  imeweza kuwafikia walengwa kwa asilimia 70 ya Mitaa, vijiji na sheia kwa Zanzibar na kwamba lengo la Serikali ni kumaliza asilimia 30 ya sehemu zilizobaki hivyo hadi kufikia  mwakani mpango wa pili wa TASAF 111 ambao sasa unaandaliwa  utakuwa umekamilika.

Akizungumzia kuhusu ucheleweshaji wa malipo ya ajira za muda amesema kuwa tatizo kubwa ilikuwa ni mfumo ambapo kama taarifa za waliofanya kazi ya ajira za muda  hazijaingiizwa kwenye mfumo huwezi kulipa hadi halmshauri zote ziwe zimeshaingiza lakini TASAF imekubaliana na wadau wa Maendeleo na Serikali kuwa kama sehemu imechelewa kuingiza taarifa wengine wasicheleshwe malipo

Ameongeza kuwa kwa wanafunzi waliopo kwenye kaya za mpango na hawakubahatika kuchaguliwa kujiunga na masomo ya Sekondari TASAF bado inawaangalia na wanaweza kusaidiwa ada kujiunga kwenye ufundi pamoja na fedha ya kujikimu kwenye majukumu mengine kama ununuzi wa nguo n.k..Na kwa watu wenye ulemavu ambao hawawezi kufanya kazi za ajira za muda TASAF  itaangalia namna nzuri  ili na wao waweze kunufaika.

Nae Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa Mtwara-Mikindani Ernest Mwongi amewashukuru TASAF kwa juhudi wanazozifanya kwa kuwasaidia Wananchi  kwani imepunguza mzigo kwa halmashauri kwa kuwa kuna mambo mengine yalitakiwa yafanywe na Manispaa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mtaa wa Chipuputa Hamisi Chambea ameshukuru kwa mtaa wake kufikiwa na TASAF na wananchi wake wamenufaika na ajira za muda na wamejenga mifereji na kwamba wao kama viongozi wako imara katika kuusimamia mradi.

Awali akisoma taarifa ya utekelezaji wa mpango wa kunusuru kaya masikini katika Mtaa wa Chipuputa Afisa mtendaji wa Mtaa huo Henry Lupapa amesema kuwa Chipuputa ina walengwa 118 ambao wananufaika na mpango..Amesema kuwa shilingi milioni 81,160,230 zimehaulishwa kuanzia kipindi cha Machi-April 2014 hadi sasa, na jumla ya awamu 23 za malipo zimefanyika. Pia jumla ya shilingi 25, 944,400 zimehaulishwa kupitia miradi ya ajira za muda kuanzia mwezi Januari 2015 hadi sasa. Vikundi vya kuweka akiba na kuwekeza vilivyopata ruzuku ni pamoja na kikundi cha Amani, Imani, Hapa kazi, Azimio, kubali  na ushirikiano na kila kikundi kimepata ruzuku ya shilingi 300,000.

Matangazo

  • Taarifa Kwa Umma ya Ilani ya Kuondoka Kwenye Kiwanja Nmaba 1-149 Litingi January 03, 2025
  • Taarifa Kwa Umma Ufafanuzi Kuhusu Jina la Shule ya Sekondari Mwalimu Nyange January 02, 2025
  • Terms Of Reference For The Provisions Of Construction Supervision Consultancy Services For Urban Infrastructures Development In Mtwara Mikindani Municipality Under The TACTIC Project March 07, 2025
  • Tangazo la Kuitwa Kwenye Usaili Nafasi ya Mwandikishaji Msaidizi na BVR Operators January 09, 2025
  • Tazama yote

Habari mpya

  • Kamati ya Siasa Mkoa Yapongeza Utekeelzaji wa Miradi ya MaendeleoMtwara-Mikindani

    January 08, 2025
  • MD Nyange Ateta na Watumishi Wa Kada ya Afya

    January 07, 2025
  • Vikundi Vilivyopata Mkopo Vyahimizwa Kurejesha Fedha Kwa Wakati

    January 06, 2025
  • Mtwara-Mikindani Yatoa Mkopo wa Mil.640.9 Kwa Vikundi 58

    January 06, 2025
  • Tazama yote

Video

Namna ya Kujisajili na Kutumia mfumo wa Uhamisho kwa watumishi wa Umma
Video nyinginezo

Viunganishi vya haraka

  • Zabuni ya ujenzi wa barabara km 4.1,Ujenzi wa Mfereji wa maji ya mvua toka Skoya,nabwada hadi Mtepwezi,Ujenzi wa soko la Chuno,Ukarabati wa stendi ya Mikindani pamoja na Uboreshaji wa sehemu za kupumzikia na michezo
  • Kupata matokeo ya Darasa la nne 2017 Manispaa Mtwara-Mikindani
  • Matokeo ya Kidato cha Pili 2017 Manispaa Mtwara-Mikindani
  • Taratibu za Kupata fomu za Vileo

Viunganishi linganifu

  • Tovuti kuu ya Serikali
  • OR - TAMISEMI
  • Wakala ya Serikali Mtandao
  • Utumishi wa Umma
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Takwimu ya Taifa

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    Manispaa Mtwara-Mikindani

    Anuani ya Posta: P. o. Box 92,

    Simu ya mezani: 023-2333102

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.