• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mtwara Mikindani Municipal Council
Mtwara Mikindani Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Manispaa ya Mtwara Mikindani

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Idara
      • Elimu ya Sekondari
      • Elimu ya Msingi
      • Idara ya Maji
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na biashara
      • Afya
      • Usafi na Mazingira
      • Ujenzi
      • Mipango Miji, Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ufugaji na Uvuvi
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
    • Kitengo
      • Ukaguzi wa ndani
      • Teknolojia, Habari, Mawasiliano na Mahusiano
      • Manunuzi na Ugavi
        • Fursa za Uwekezaji
          • Vivutio vya Utalii
          • Maeneo ya Viwanda
      • Ufugaji wa nyuki
      • Uchaguzi
      • Sheria
    • Muundo wa Kiutawala
    • Kata
      • Shangani
      • Rahaleo
      • Reli
      • Vigaeni
      • Majengo
      • Magomeni
      • Ufukoni
      • Mitengo
      • Magengeni
      • Mtonya
      • Kisungule
      • Jangwani
      • Mtawanya
      • Naliendele
      • Chikongola
      • Chuno
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Maeneo ya Viwanda
  • Huduma
    • huduma za maji
    • Huduma za afya
    • Huduma za elimu
    • HUduma za watumishi
    • Uzoaji wa taka ngumu
  • Madiwani
    • Orodha ya Wahe. Wabunge na Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipangomiji na Ujenzi
      • Huduma za Jamii
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Ratiba za Vikao
      • Kumuona Mstahiki Meya
  • Mradi
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi mipya
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Miongozo
    • Fomu
    • Huduma kwa Mteja
    • Ripoti
    • Mpango Mkakati
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Videos
    • Hotuba
    • Maktaba cha Picha

TPDC Yakabidhi Miradi ya Mil.30 kwa Shule za Shangani, Rahaleo

Posted on: July 16th, 2020





Katika kuhakikisha kuwa wanafunzi wananufaika na uwepo wa gesi asilia katika Mikoa ya Mtwara na Lindi, Shirika la Maendeleo ya Petrol nchini (TPDC) limetumia shilingi Milioni 30,052,500 Kujenga choo cha wanafunzi wenye mahitaji maalumu shule ya Msingi Shangani, Kukarabati vyoo na uchimbaji wa kisima cha maji katika shule ya Msingi ya Rahaleo  zilizopo Manispaa ya Mtwara-Mikindani.

Katifa fedha hizo shilingi Milioni18,600,000 zimetumika kujenga matundu ya vyoo shule ya Msingi Shangani na shilingi Milioni 14,452,500 zimetumika kukarabati matundu ya choo cha wasichana na uchimbaji wa kisima cha maji shule ya Msingi Rahaleo.

Akizungumza katika hafla fupi ya kukabidhi miradi hiyo iliyofanyika Julai 16,2020, Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe Dunstan Kyobya amepongeza uongozi ya TPDC kwa kuguswa na kuamua kujitoa kujenga vyoo kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu na kwa wanafunzi wasichana wa shule hizo.

Pamoja na pongezi hizo pia Kyobya amewataka wadau mbalimbali wa maendeleo  waliopo Mtwara kuunga mkono jitihada za Serikali na kufuata nyayo za TPDC kwa  kujitoa na kuchangia katika sekta ya elimu ili Wanafunzi wasome katika mazingira mazuri.

Aidha Kyobya ametoa wito kwa wazazi na walezi wenye Watoto wenye mahitaji maalumu (walemavu) kuhakikisha kuwa Watoto hao hawakai nyumbani badala yake wapelekwe shuleni kwa ajili ya kupata Elimu kama Watoto wengine na kuwataka walimu kutoa taarifa katika vyombo husika endapo kuna mwanafnzi haudhurii masomo(utoro).

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani Bi Juliana Manyama amewashukuru Shirika hilo kwa msaada walioutoa na kuwaomba kuendelea kusaidia katika shule zingine kwa kuwa mahitaji yako mengi.

Nae Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Shirika la Maendeleo ya Petrol nchini Bi. Marie Mselem amesema kuwa Shirika hilo limeweka utaratibu wa kurudisha kwa jamii kwa kuchangia katika sekta ya elimu, afya na utawala bora hivyo ujenzi wa choo bora kwa Watoto wenye mahitaji maalumu itawapelekea Watoto hao kusoma vizuri na kupenda kwenda shule.

Awali akisoma taarifa ya Shule Mwalimu MKuu wa Shule ya Msingi Shangani Bi. Marylce Elisha amesema kuwa jumla ya wanafunzi sabini na tano watanufaika na choo hiko na kuwashukuru Shirika hilo kuendelea kuchangia katika Shule kwa kuwa wanachangamoto nyingi ikiwemo uchakavu wa madarasa.

Matangazo

  • Taarifa Kwa Umma ya Ilani ya Kuondoka Kwenye Kiwanja Nmaba 1-149 Litingi January 03, 2025
  • Taarifa Kwa Umma Ufafanuzi Kuhusu Jina la Shule ya Sekondari Mwalimu Nyange January 02, 2025
  • Terms Of Reference For The Provisions Of Construction Supervision Consultancy Services For Urban Infrastructures Development In Mtwara Mikindani Municipality Under The TACTIC Project March 07, 2025
  • Tangazo la Kuitwa Kwenye Usaili Nafasi ya Mwandikishaji Msaidizi na BVR Operators January 09, 2025
  • Tazama yote

Habari mpya

  • Kamati ya Siasa Mkoa Yapongeza Utekeelzaji wa Miradi ya MaendeleoMtwara-Mikindani

    January 08, 2025
  • MD Nyange Ateta na Watumishi Wa Kada ya Afya

    January 07, 2025
  • Vikundi Vilivyopata Mkopo Vyahimizwa Kurejesha Fedha Kwa Wakati

    January 06, 2025
  • Mtwara-Mikindani Yatoa Mkopo wa Mil.640.9 Kwa Vikundi 58

    January 06, 2025
  • Tazama yote

Video

Namna ya Kujisajili na Kutumia mfumo wa Uhamisho kwa watumishi wa Umma
Video nyinginezo

Viunganishi vya haraka

  • Zabuni ya ujenzi wa barabara km 4.1,Ujenzi wa Mfereji wa maji ya mvua toka Skoya,nabwada hadi Mtepwezi,Ujenzi wa soko la Chuno,Ukarabati wa stendi ya Mikindani pamoja na Uboreshaji wa sehemu za kupumzikia na michezo
  • Kupata matokeo ya Darasa la nne 2017 Manispaa Mtwara-Mikindani
  • Matokeo ya Kidato cha Pili 2017 Manispaa Mtwara-Mikindani
  • Taratibu za Kupata fomu za Vileo

Viunganishi linganifu

  • Tovuti kuu ya Serikali
  • OR - TAMISEMI
  • Wakala ya Serikali Mtandao
  • Utumishi wa Umma
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Takwimu ya Taifa

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    Manispaa Mtwara-Mikindani

    Anuani ya Posta: P. o. Box 92,

    Simu ya mezani: 023-2333102

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.