• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mtwara Mikindani Municipal Council
Mtwara Mikindani Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Manispaa ya Mtwara Mikindani

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Idara
      • Elimu ya Sekondari
      • Elimu ya Msingi
      • Idara ya Maji
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na biashara
      • Afya
      • Usafi na Mazingira
      • Ujenzi
      • Mipango Miji, Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ufugaji na Uvuvi
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
    • Kitengo
      • Ukaguzi wa ndani
      • Teknolojia, Habari, Mawasiliano na Mahusiano
      • Manunuzi na Ugavi
        • Fursa za Uwekezaji
          • Vivutio vya Utalii
          • Maeneo ya Viwanda
      • Ufugaji wa nyuki
      • Uchaguzi
      • Sheria
    • Muundo wa Kiutawala
    • Kata
      • Shangani
      • Rahaleo
      • Reli
      • Vigaeni
      • Majengo
      • Magomeni
      • Ufukoni
      • Mitengo
      • Magengeni
      • Mtonya
      • Kisungule
      • Jangwani
      • Mtawanya
      • Naliendele
      • Chikongola
      • Chuno
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Maeneo ya Viwanda
  • Huduma
    • huduma za maji
    • Huduma za afya
    • Huduma za elimu
    • HUduma za watumishi
    • Uzoaji wa taka ngumu
  • Madiwani
    • Orodha ya Wahe. Wabunge na Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipangomiji na Ujenzi
      • Huduma za Jamii
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Ratiba za Vikao
      • Kumuona Mstahiki Meya
  • Mradi
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi mipya
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Miongozo
    • Fomu
    • Huduma kwa Mteja
    • Ripoti
    • Mpango Mkakati
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Videos
    • Hotuba
    • Maktaba cha Picha

DC Mtwara atangaza Vita dhidi ya wanaowapa ujauzito Wanafunzi

Posted on: March 8th, 2018

Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Evod Mmanda akiagana  na Wanafunzi mara baada ya kufunga shughuli za maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani zilizofanyika tarehe 8 Machi katika Viwanja vya Mashujaa.


Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe.Evod Mmanda jana kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani yaliyofanyika kwenye Viwanja  vya Mashujaa Manispaa Mtwara Mikindani ametangaza vita kwa wale wote watakaobainika kuwapa ujauzito watoto wa kike na kuwakatisha masomo yao.

Amesema kuwa vita hiyo haitaishia kwa wavulana tu hata  wanafunzi wa kike watakaobainika kuwa na ujauzito na wazazi au walezi watakaomfumbia macho kijana aliempa ujauzito binti huyo wote watashughulikiwa  kwa mujibu wa sheria.

“Mabinti mnaosoma na kupata ujauzito hata nyinyi tutakabana labda uwe umebakwa na unaripoti ya Polisi hapo tutashughulika  na yule aliyebaka wewe utapata ushauri nasaha, tiba na matunzo mazuri kwa sababu umepata ajali kubwa iliyodhuru mwili wako.

“Na kwa Mzazi ambae binti yake amepata ujauzito badala ya kumbaini kijana mnakaa pande mbili kupatana kama munauziana viwanja kumficha aliyetia ujauzito huku aliyetiwa mimba anaendelea kuteseka na kuwa mzazi asiye na Matunzo  tutahangaika na wewe   na kwa hili sitatania” alisema Mmanda

Mkuu wa Wilaya ya Mtwara akikabidhi zawadi kwa mmoja wa wanafunzi wanaofanya vizuri darasani kwneye masomo ya sayansi

Aidha Mmanda ametoa onyo kwa kwa watoto wa kike wanaotumia uzazi wa mpango ili kujikinga na  mimba  pindi wakiwa shuleni,  pia onyo hilo limetolewa na kwa wazazi na manesi wanaowasaidia watoto hao kuwapa uzazi wa mpango.

“Ole wako wewe mzazi, ole wako wewe nesi unaehusika na zoezi kama hili kwa sababu unafikiri unamsaidia mtoto, unapompa uzazi wa mpango maana yake una tambua ana mahusiano sasa unamuambia mwanangu asante jembe hili lima vizuri matokeo yake unamuingiza kwenye kazi mbili shule na mapenzi.

“ninawaambia utazuia mimba lakini si ukimwi na magonjwa ya zinaa kwa sababu ni ishara kuwa ngono zembe inafanyika kwa kutumia uzazi wa mpango maana yake yuko huru, yupo kwenye bahari ya Hindi aogelee kwa nguvu zake hata akifika Msumbiji haya ni matatizo.” Amesema Mmanda

Adha amewataka watoto wa kike kusoma kwa bidii na kutokuwa haraka kwani wanavyoendelea kusonga mbele kielimu ndivyo wanavyojihakikishia kupata Uhakika wa maisha mazuri na kupata mume bora zaidi. Amesema kuwa anatambua wanawake wana jukumu kubwa la kuringa na kujidai kwa majukumu makubwa waliyonayo ya kifamilia na Taifa kwa ujumla.

Siku ya Wanawake Duniani hufanyika kila mwaka Ifikapo tarehe 8 Machi na kwa Manispaa Mtwara-Mikindani maadhimisho haya yaliambatana  na ugawaji wa Bima za afya kwa watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi, ugawaji wa zawadi kwa watoto wa kike wanaofanya vizuri darasani kwneye masomo ya sayansi, kufanya mazungumzo na watoto wa kike wanaosoma Shule za Sekondari ili kuwatia moyo, Ugawaji wa zawadi kwa wagonjwa waliolazwa Zahanati ya Likombe na kufanya usafi  katika zahanati hiyo pamoja na maonesho ya wajasiriamaliali yaliyofanyika kwenye viwanja vya Mashujaa. Aidha kauli mbiu ya mwaka huu inasema“KUELEKEA UCHUMI WA VIWANDA  TUIMARISHE USAWA WA JINSIA NA UWEZESHAJI WA WANAWAKE VIJIJINI”.



Matangazo

  • Taarifa Kwa Umma ya Ilani ya Kuondoka Kwenye Kiwanja Nmaba 1-149 Litingi January 03, 2025
  • Taarifa Kwa Umma Ufafanuzi Kuhusu Jina la Shule ya Sekondari Mwalimu Nyange January 02, 2025
  • Terms Of Reference For The Provisions Of Construction Supervision Consultancy Services For Urban Infrastructures Development In Mtwara Mikindani Municipality Under The TACTIC Project March 07, 2025
  • Tangazo la Kuitwa Kwenye Usaili Nafasi ya Mwandikishaji Msaidizi na BVR Operators January 09, 2025
  • Tazama yote

Habari mpya

  • Kamati ya Siasa Mkoa Yapongeza Utekeelzaji wa Miradi ya MaendeleoMtwara-Mikindani

    January 08, 2025
  • MD Nyange Ateta na Watumishi Wa Kada ya Afya

    January 07, 2025
  • Vikundi Vilivyopata Mkopo Vyahimizwa Kurejesha Fedha Kwa Wakati

    January 06, 2025
  • Mtwara-Mikindani Yatoa Mkopo wa Mil.640.9 Kwa Vikundi 58

    January 06, 2025
  • Tazama yote

Video

Namna ya Kujisajili na Kutumia mfumo wa Uhamisho kwa watumishi wa Umma
Video nyinginezo

Viunganishi vya haraka

  • Zabuni ya ujenzi wa barabara km 4.1,Ujenzi wa Mfereji wa maji ya mvua toka Skoya,nabwada hadi Mtepwezi,Ujenzi wa soko la Chuno,Ukarabati wa stendi ya Mikindani pamoja na Uboreshaji wa sehemu za kupumzikia na michezo
  • Kupata matokeo ya Darasa la nne 2017 Manispaa Mtwara-Mikindani
  • Matokeo ya Kidato cha Pili 2017 Manispaa Mtwara-Mikindani
  • Taratibu za Kupata fomu za Vileo

Viunganishi linganifu

  • Tovuti kuu ya Serikali
  • OR - TAMISEMI
  • Wakala ya Serikali Mtandao
  • Utumishi wa Umma
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Takwimu ya Taifa

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    Manispaa Mtwara-Mikindani

    Anuani ya Posta: P. o. Box 92,

    Simu ya mezani: 023-2333102

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.