Manispaa ya Mtwara-Mikindani tupo kwenye kilele cha Tamasha la Msangamkuu (MsangaMkuu Beach Festival) ) Leo Desemba 31,2024.
Tunawakaribisha wananchi wanaotembelea kwenye Tamasha hili kutembelea banda letu kwa ajili ya kujifunza mambo mengi mazuri yahusuyo utamaduni wa kabila la wamakonde, wayao na wamwela pamoja na kuona na kujifunza kazi za sanaa za uchoraji,uchongaji,ususi na ushonaji.
Aidha tunawakaribisha kuja kujipatia kiwanja katika Mji wa kisasa wa "SAMIA CITY" ili uweze kufunga na kufungua mwaka Kwa kujipatia makazi Bora na endelevu.
Pia tunatoa huduma mbalimbali za afya ikiwemo uchangiaji damu, Upimaji wa VVU.
Tamasha la Msangamkuu limelenga kuhamasisha Uwekezaji kwenye fukwe za bahari.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.