• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mtwara Mikindani Municipal Council
Mtwara Mikindani Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Manispaa ya Mtwara Mikindani

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Idara
      • Elimu ya Sekondari
      • Elimu ya Msingi
      • Idara ya Maji
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na biashara
      • Afya
      • Usafi na Mazingira
      • Ujenzi
      • Mipango Miji, Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ufugaji na Uvuvi
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
    • Kitengo
      • Ukaguzi wa ndani
      • Teknolojia, Habari, Mawasiliano na Mahusiano
      • Manunuzi na Ugavi
        • Fursa za Uwekezaji
          • Vivutio vya Utalii
          • Maeneo ya Viwanda
      • Ufugaji wa nyuki
      • Uchaguzi
      • Sheria
    • Muundo wa Kiutawala
    • Kata
      • Shangani
      • Rahaleo
      • Reli
      • Vigaeni
      • Majengo
      • Magomeni
      • Ufukoni
      • Mitengo
      • Magengeni
      • Mtonya
      • Kisungule
      • Jangwani
      • Mtawanya
      • Naliendele
      • Chikongola
      • Chuno
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Maeneo ya Viwanda
  • Huduma
    • huduma za maji
    • Huduma za afya
    • Huduma za elimu
    • HUduma za watumishi
    • Uzoaji wa taka ngumu
  • Madiwani
    • Orodha ya Wahe. Wabunge na Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipangomiji na Ujenzi
      • Huduma za Jamii
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Ratiba za Vikao
      • Kumuona Mstahiki Meya
  • Mradi
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi mipya
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Miongozo
    • Fomu
    • Huduma kwa Mteja
    • Ripoti
    • Mpango Mkakati
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Videos
    • Hotuba
    • Maktaba cha Picha

Vijana, Wanawake Mtwara-Mikindani Wapokea MIL. 154.1

Posted on: November 28th, 2017

VIJANA NA WANAWAKE MTWARA-MIKINDANI WAPOKEA MILIONI 154.1

Katika kutekeleza agizo la Serikali  lililotaka halmashauri zote nchini kutenga asilimia 10 ya mapato yake ya ndani kwa ajili ya kuwezesha vikundi vya wanawake na vijana Halmashauri ya Manispaa Mtwara-Mikindani imeendelea kuneemesha vikundi vya wajasiriamali hao  kwa kuwapatia mkopo wa shilingi milioni 154,180,000 kwa awamu ya kwanza.

Mkopo huo uliotolewa kwa vikundi 48 vya wanawake na Vijana kupitia mfuko wa Wananwake naVijana(WDF) umelenga kuwasaidia wajasiriamali hao kukuza mitaji yao ili waweze kujikwamua kiuchumi.

Akizungumza kwenye hafla fupi ya kukabidhi mfano wa  hundi kwa wanavikundi hao iliyofanyika kwenye ukumbi wa boma mkoa Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mh.Evod Mmanda amewataka  wanavikundi   kutumia mkopo waliopewa  kwa weledi na maarifa ya kutosha.

Amesema kuwa ili mkopo uwe na tija kwenye familia zao ni lazima wanavikundi hao waangalie shughuli wanazozifanya na kutafakari kama shughuli hizo zinafaida kiuchumi au la ili waweze kutafuta shughuli mbadala.

Pia amewaasa wanavikundi hao kutotumia mkopo nje ya malengo kwani kutumika  nje ya malengo  inaletwa taswira ya kuwa wanavikundi hao hawakujipanga na watashindwa kurejesha kwa wakati hali itakayopelekea watu wengine fursa ya kupata mikopo.

MManda amesema  kuwa wakati Tanzania  ikielekea kwenye viwanda wajasiriamalia mali hao wajipange kwa ajili ya kupata ajira kwa wageni watakaokuja kujenga viwanda lakini ni fursa kwao kwakutengeza bidhaa nzuri kama nguo, kupika chakula kwa mama lishe na uzoaji wa taka zinazozalishwa. Aidha amewataka waboreshe huduma zao ili waweze kupata fursa zaidi.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa Bi Beatrice Dominic amesema kuwa Manispaa kwa sasa inaangalia vikundi vya akina mama ambao tayari wapo kwenye viwanda vidogo ili iwatafutie eneo na kuwaweka pamoja kwa ajili ya kuuza bidhaa zao. Hivyo amewataka wajipange kw a ajili ya kuingia kwenye aina nyingine ya ujasiriamali ya viwanda vidogovidogo.

Nae  chilumba mwakilishi wa vijana ameishukuru serikali ya Tanzania kwa kuwajali na na kwamba atahamasisha viana wengine ili waweze kujiunga kwenyevikundi na kupatiwa mikopo lakini amewataka wajasiriamal wengine waliopewa mikopokurejesha fedha kwa wakati.

Awali akisoma taarifa ya Mikopo hiyo Afisa Maendeleo ya Jamii Juliana Manyama alisema  kuwa  Vikundi vilivyoomba mkopo vilikuwa 88 vyenye jumla shilingi 453,000,000 lakini baada ya uchambuzi vikundi vilivyokidhi vigezo ni 78 vyenye jumla ya shilingi 291,684,300. Hata hivyo mkopo uliotolewa  wa shilngi milioni ni 154,180,000 ni awamu ya kwanza kwa vikundi  48 vikiwemo vya wanawake 40 na vijana 8 na kufanya wanufaika wa mkopo huo kuwa 240.

 Kwa mwaka wa fedha 2017/2018 Manispaa imetenga Shilingi milioni 487,514,286 kwa ajili ya mfuko wa Wanawake na Vijana(WDF) ambayo ni sawa na Asilimia 10 ya mapato ya ndani na itanufaisha vikundi 110.

Matangazo

  • Taarifa Kwa Umma ya Ilani ya Kuondoka Kwenye Kiwanja Nmaba 1-149 Litingi January 03, 2025
  • Taarifa Kwa Umma Ufafanuzi Kuhusu Jina la Shule ya Sekondari Mwalimu Nyange January 02, 2025
  • Terms Of Reference For The Provisions Of Construction Supervision Consultancy Services For Urban Infrastructures Development In Mtwara Mikindani Municipality Under The TACTIC Project March 07, 2025
  • Tangazo la Kuitwa Kwenye Usaili Nafasi ya Mwandikishaji Msaidizi na BVR Operators January 09, 2025
  • Tazama yote

Habari mpya

  • Kamati ya Siasa Mkoa Yapongeza Utekeelzaji wa Miradi ya MaendeleoMtwara-Mikindani

    January 08, 2025
  • MD Nyange Ateta na Watumishi Wa Kada ya Afya

    January 07, 2025
  • Vikundi Vilivyopata Mkopo Vyahimizwa Kurejesha Fedha Kwa Wakati

    January 06, 2025
  • Mtwara-Mikindani Yatoa Mkopo wa Mil.640.9 Kwa Vikundi 58

    January 06, 2025
  • Tazama yote

Video

Namna ya Kujisajili na Kutumia mfumo wa Uhamisho kwa watumishi wa Umma
Video nyinginezo

Viunganishi vya haraka

  • Zabuni ya ujenzi wa barabara km 4.1,Ujenzi wa Mfereji wa maji ya mvua toka Skoya,nabwada hadi Mtepwezi,Ujenzi wa soko la Chuno,Ukarabati wa stendi ya Mikindani pamoja na Uboreshaji wa sehemu za kupumzikia na michezo
  • Kupata matokeo ya Darasa la nne 2017 Manispaa Mtwara-Mikindani
  • Matokeo ya Kidato cha Pili 2017 Manispaa Mtwara-Mikindani
  • Taratibu za Kupata fomu za Vileo

Viunganishi linganifu

  • Tovuti kuu ya Serikali
  • OR - TAMISEMI
  • Wakala ya Serikali Mtandao
  • Utumishi wa Umma
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Takwimu ya Taifa

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    Manispaa Mtwara-Mikindani

    Anuani ya Posta: P. o. Box 92,

    Simu ya mezani: 023-2333102

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.