• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mtwara Mikindani Municipal Council
Mtwara Mikindani Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Manispaa ya Mtwara Mikindani

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Idara
      • Elimu ya Sekondari
      • Elimu ya Msingi
      • Idara ya Maji
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na biashara
      • Afya
      • Usafi na Mazingira
      • Ujenzi
      • Mipango Miji, Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ufugaji na Uvuvi
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
    • Kitengo
      • Ukaguzi wa ndani
      • Teknolojia, Habari, Mawasiliano na Mahusiano
      • Manunuzi na Ugavi
        • Fursa za Uwekezaji
          • Vivutio vya Utalii
          • Maeneo ya Viwanda
      • Ufugaji wa nyuki
      • Uchaguzi
      • Sheria
    • Muundo wa Kiutawala
    • Kata
      • Shangani
      • Rahaleo
      • Reli
      • Vigaeni
      • Majengo
      • Magomeni
      • Ufukoni
      • Mitengo
      • Magengeni
      • Mtonya
      • Kisungule
      • Jangwani
      • Mtawanya
      • Naliendele
      • Chikongola
      • Chuno
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Maeneo ya Viwanda
  • Huduma
    • huduma za maji
    • Huduma za afya
    • Huduma za elimu
    • HUduma za watumishi
    • Uzoaji wa taka ngumu
  • Madiwani
    • Orodha ya Wahe. Wabunge na Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipangomiji na Ujenzi
      • Huduma za Jamii
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Ratiba za Vikao
      • Kumuona Mstahiki Meya
  • Mradi
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi mipya
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Miongozo
    • Fomu
    • Huduma kwa Mteja
    • Ripoti
    • Mpango Mkakati
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Videos
    • Hotuba
    • Maktaba cha Picha

Wafanyabiashara Soko la Chuno Waombwa kuwa watulivu

Posted on: May 7th, 2021

Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani  COL. Emanuel Mwaigobeko   amewataka wafanyabiashara wa Soko la Chuno kuwa watulivu  katika kipindi hiki wakati Serikali ikiendelea  kushughulikia  mgogoro kati ya wafanyabiashara  wa soko  la sabasaba na  Manispaa  ili kupisha taratibu za kimahakama zinazoendelea.

Mkurugenzi ametoa rai hiyo  katika kikao chake na wafanyabiashara wa Soko la chuno  kilichofanyika  mapema leo tarehe 7 Mei 2021  katika viunga vya soko la chuno Mkoani lililopo Manispaa ya Mtwara-Mikindani.

Amesema kuwa ,  Serikali inaendelea na taratibu stahiki  za kimahakama katika kushughulikia mgogoro huo na  kesi ipo katika hatua za mwisho, hivyo wafanyabiashara hao wanatakiwa kuwa watulivu  na kuendelea na majukumu yao ya kila siku sokoni  hapo wakisubiria hatma ya  kesi hiyo.

“Naomba nitoe rai ndugu zangu  pamoja na ukimya uliopo  kesi tayari ipo mahakamani  inasikilizwa sio kwamba tumekaa kimya  tunapisha  taratibu za kimahakama hivyo niwaombe  tuwe watulivu wakati taratibu hizo zikifuatwa”alisema Mwaigobeko

Aidha amemtaka mwenyekiti wa soko la chuno Bw. Ally Ndale   kuchukua orodha ya vizimba  vilivyo wazi  (visivyo na biashara)   na  kutafuta utaratibu maalum  wa kuvigawa kwa  wafanyabiashara wa soko hilo ambao wamekosa vizimba ili waweze kuendesha biashara zao kwa maslahi  yao  binafsi na  ya Halmashauri kwa ujumla.

“Nikuagize Mwenyekiti wa  Soko la Chuno, orodhesha  vizimba vilivyo wazi  ambavyo havina biashara na uvigawe kwa wafanya biashara ambao hawana vizimba hatuwezi kuona  vizimba vipo wazi  mwenye chake amestarehe nyumbani wakati mfanyabiashara mwingine anahangaika hana sehemu ya kufanyia biashara’’alisema Mwaigobeko

Naye Mstahiki Meya  wa Manispaa ya Mtwara-Mkindani   Shadida Ndile  amesikitishwa na taratibu zinazoendelea kufanywa na wafanyabiashara wa soko la saba saba  ikiwa na pamoja  na kuleta vurugu  katika maeneo ya soko la Chuno  na amewataka waache mara moja na kujikita Zaidi katika biashara zao wakati  mahakama  ikishughulikia  mgogoro huo.

“Nimesikitishwa na taratibu tunazoendelea nazo wana mtwara, misuguano na migogoro tunayoifanya haina tija  inarudisha nyuma maendeleo katika Manispaa  yetu,mwekezaji hawezi kuja kuwekeza mahali ambapo pana migogoro, tunadumaza maendeleo yetu wenyewe , tujirekebishe  na tuendelee kufanya kazi zetu kwa weledi  kwa manufaa ya Taifa kwa ujumla”alisema Shadida

Awali Mwenyekiti wa Soko la Chuno Bw. Ali Ndale amemshukuru Mkrugenzi wa Halmashauri ya Mtwara-Mikindani kwa kukubali wito wa kuzungumza nao na  kwa niaba ya wafanyabiashara wa soko la chuno ameomba  kupata mrejesho wa kesi kati ya wafanya biashara ya Chuno na Sabasaba.

Matangazo

  • Taarifa Kwa Umma ya Ilani ya Kuondoka Kwenye Kiwanja Nmaba 1-149 Litingi January 03, 2025
  • Taarifa Kwa Umma Ufafanuzi Kuhusu Jina la Shule ya Sekondari Mwalimu Nyange January 02, 2025
  • Terms Of Reference For The Provisions Of Construction Supervision Consultancy Services For Urban Infrastructures Development In Mtwara Mikindani Municipality Under The TACTIC Project March 07, 2025
  • Tangazo la Kuitwa Kwenye Usaili Nafasi ya Mwandikishaji Msaidizi na BVR Operators January 09, 2025
  • Tazama yote

Habari mpya

  • Kamati ya Siasa Mkoa Yapongeza Utekeelzaji wa Miradi ya MaendeleoMtwara-Mikindani

    January 08, 2025
  • MD Nyange Ateta na Watumishi Wa Kada ya Afya

    January 07, 2025
  • Vikundi Vilivyopata Mkopo Vyahimizwa Kurejesha Fedha Kwa Wakati

    January 06, 2025
  • Mtwara-Mikindani Yatoa Mkopo wa Mil.640.9 Kwa Vikundi 58

    January 06, 2025
  • Tazama yote

Video

Namna ya Kujisajili na Kutumia mfumo wa Uhamisho kwa watumishi wa Umma
Video nyinginezo

Viunganishi vya haraka

  • Zabuni ya ujenzi wa barabara km 4.1,Ujenzi wa Mfereji wa maji ya mvua toka Skoya,nabwada hadi Mtepwezi,Ujenzi wa soko la Chuno,Ukarabati wa stendi ya Mikindani pamoja na Uboreshaji wa sehemu za kupumzikia na michezo
  • Kupata matokeo ya Darasa la nne 2017 Manispaa Mtwara-Mikindani
  • Matokeo ya Kidato cha Pili 2017 Manispaa Mtwara-Mikindani
  • Taratibu za Kupata fomu za Vileo

Viunganishi linganifu

  • Tovuti kuu ya Serikali
  • OR - TAMISEMI
  • Wakala ya Serikali Mtandao
  • Utumishi wa Umma
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Takwimu ya Taifa

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    Manispaa Mtwara-Mikindani

    Anuani ya Posta: P. o. Box 92,

    Simu ya mezani: 023-2333102

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.