• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mtwara Mikindani Municipal Council
Mtwara Mikindani Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Manispaa ya Mtwara Mikindani

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Idara
      • Elimu ya Sekondari
      • Elimu ya Msingi
      • Idara ya Maji
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na biashara
      • Afya
      • Usafi na Mazingira
      • Ujenzi
      • Mipango Miji, Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ufugaji na Uvuvi
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
    • Kitengo
      • Ukaguzi wa ndani
      • Teknolojia, Habari, Mawasiliano na Mahusiano
      • Manunuzi na Ugavi
        • Fursa za Uwekezaji
          • Vivutio vya Utalii
          • Maeneo ya Viwanda
      • Ufugaji wa nyuki
      • Uchaguzi
      • Sheria
    • Muundo wa Kiutawala
    • Kata
      • Shangani
      • Rahaleo
      • Reli
      • Vigaeni
      • Majengo
      • Magomeni
      • Ufukoni
      • Mitengo
      • Magengeni
      • Mtonya
      • Kisungule
      • Jangwani
      • Mtawanya
      • Naliendele
      • Chikongola
      • Chuno
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Maeneo ya Viwanda
  • Huduma
    • huduma za maji
    • Huduma za afya
    • Huduma za elimu
    • HUduma za watumishi
    • Uzoaji wa taka ngumu
  • Madiwani
    • Orodha ya Wahe. Wabunge na Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipangomiji na Ujenzi
      • Huduma za Jamii
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Ratiba za Vikao
      • Kumuona Mstahiki Meya
  • Mradi
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi mipya
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Miongozo
    • Fomu
    • Huduma kwa Mteja
    • Ripoti
    • Mpango Mkakati
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Videos
    • Hotuba
    • Maktaba cha Picha

Watumishi Waaswa Kuacha Kutumia Migomo na Vurugu katika Kudai Haki

Posted on: May 1st, 2017

Watumishi Waaswa Kuacha Kutumia Migomo na Vurugu katika Kudai Haki

Watumishi mkoani Mtwara wametakiwa kufuata sheria na taratibu katika kudai haki badala ya kuwekeza muda na nguvu zao kwenye migomo na vurugu kwani sehemu yoyote yenye vurugu hakuna mafanikio.

Hayo yamesemwa jana na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mh. Halima Dendego wakati akitoa hutuba yake kwenye sherehe za Mei Mosi zilizofanyika kwenye viwanja wa mashujaa vilivyopo Mkoani Mtwara.

Dendego amesema kuwa kwa kuwa watumishi wengi wapo kwenye vyama vya Wafanyakazi wawe makini kwenye kuchagua viongozi makini na wenye uelewa mpana na wenye uwezo wa kushawishi ili kuwawakilisha kwenye vikao vya majadiliano na kudai haki.

Aidha Mkuu wa Mkoa amewataka waajiri wote kufuata sheria na kutumia njia ya majadiliano kwenye kufikia makubaliono kwa watumishi wanaowaongoza ,kwani mambo yakuburuzana yameshapitwa na wakati katika dunia hii ya leo.

“Waajiri wote mkoani hakikisheni kuwa sheria za kazi zinafuatwa, waajiriwa wanapata haki zao bila figisu figisu,utulivu unakuwepo mahala pa kazi ili kuunga mkono kauli mbiu ya Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya HAPA KAZI TU”alisema Dendego

Vile vile Dendego amewataka watumishi walioko kazini na wanaosubiri ajira kujiendeleza kitaaluma ili kushiriki kwenye ushindani wa soko la ajira ndani na nje ya nchi. Aidha alikumbusha kuwa watu waache ubabaishaji kwani Mkoa umepoteza watumishi 175 katika zoezi lililoendeshwa na Taifa la uhakiki wa   vyeti na hivyo kuwataka waajiri kuchukua hatua.

“Ninaagiza Waajiri wa watumishi waliofoji vyeti hakikisheni mnatekeleza agizo la Mh Rais mara moja la kuwafuta katika orodha ya mishahara na stahili zingine”alisema Dendego.

Wakati huo huo Katibu wa TUCTA Mkoa wa Mtwara Bi Masaida Chiwinga aliiomba kuwa  Serikali Itilie maanani  maoni ya wawakilishi wa Wafanyakazi wakati wa kuandaa viwango vya mishahara kwani Tsh 100,000 ambacho ni kima cha chini kwa mtumishi wa Serikali hakitoshi kukidhi mahitaji.

Alisema kuwa Mkoa wa Mtwara walimu wanaidai Serikali kiasi cha Tsh. 1,809,090,901/= hivyo ameiomba Serikali kuendelea kupunguza madeni haya.

Sherehe za Mei Mosi zinafanyika kila mwaka ifikapi tarehe 1 Mei Dunia nzima wafanyakazi husherehekea siku hiyo. Kwa Tanzania Sherehe hizi zimeazimishwa Kitaifa Mkoani Kilimanjaro zikiwa na kauli mbiu inayosema ‘UCHUMI WA VIWANDA UZINGATIE HAKI, MASLAHI,HESHIMAYA WAFANYAKAZI’

Matangazo

  • Taarifa Kwa Umma ya Ilani ya Kuondoka Kwenye Kiwanja Nmaba 1-149 Litingi January 03, 2025
  • Taarifa Kwa Umma Ufafanuzi Kuhusu Jina la Shule ya Sekondari Mwalimu Nyange January 02, 2025
  • Terms Of Reference For The Provisions Of Construction Supervision Consultancy Services For Urban Infrastructures Development In Mtwara Mikindani Municipality Under The TACTIC Project March 07, 2025
  • Tangazo la Kuitwa Kwenye Usaili Nafasi ya Mwandikishaji Msaidizi na BVR Operators January 09, 2025
  • Tazama yote

Habari mpya

  • Kamati ya Siasa Mkoa Yapongeza Utekeelzaji wa Miradi ya MaendeleoMtwara-Mikindani

    January 08, 2025
  • MD Nyange Ateta na Watumishi Wa Kada ya Afya

    January 07, 2025
  • Vikundi Vilivyopata Mkopo Vyahimizwa Kurejesha Fedha Kwa Wakati

    January 06, 2025
  • Mtwara-Mikindani Yatoa Mkopo wa Mil.640.9 Kwa Vikundi 58

    January 06, 2025
  • Tazama yote

Video

Namna ya Kujisajili na Kutumia mfumo wa Uhamisho kwa watumishi wa Umma
Video nyinginezo

Viunganishi vya haraka

  • Zabuni ya ujenzi wa barabara km 4.1,Ujenzi wa Mfereji wa maji ya mvua toka Skoya,nabwada hadi Mtepwezi,Ujenzi wa soko la Chuno,Ukarabati wa stendi ya Mikindani pamoja na Uboreshaji wa sehemu za kupumzikia na michezo
  • Kupata matokeo ya Darasa la nne 2017 Manispaa Mtwara-Mikindani
  • Matokeo ya Kidato cha Pili 2017 Manispaa Mtwara-Mikindani
  • Taratibu za Kupata fomu za Vileo

Viunganishi linganifu

  • Tovuti kuu ya Serikali
  • OR - TAMISEMI
  • Wakala ya Serikali Mtandao
  • Utumishi wa Umma
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Takwimu ya Taifa

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    Manispaa Mtwara-Mikindani

    Anuani ya Posta: P. o. Box 92,

    Simu ya mezani: 023-2333102

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.