Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe Gelasius Byakanwa amezitaka Halmashauri zote zilizozopo Mkoani Mtwara kutenga maeneo ya wazi makubwa kwa ajili ya michezo na sehemu za watu kupumzika na kuburudika kama ambavyo Manispaa ya Mtwara-Mikindani imefanya.
Bykanwa ametoa agizo hilo Oktoba 10, 2020 alipokuwa anafanya uzinduzi wa Bustani za kupumzikia za Tilla, Maduka Makubwa na Mashujaa katika Viwanja vya Mashujaa vilivyopo Manispaa ya Mtwara-Mikindani.
Pamoja na agizo hilo Byakanwa pia amewapongeza wananchi wa Mtwara kwa kuendelea kuyatunza maeneo ya wazi yaliyopo na ameahidi kuyasimamia maeneo hayo yaliyotengwa kwa matumizi ya umma.
“Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni , Sijaona watu wakijenga maeneo ya barabara wala maeneo ya wazi, hata wale waliothubutu kuja katika ofisi yangu kunishawishi kubadilisha matumizi ya maeneo ya wazi niliwakatalia, kwenye suala la la usimamaizi wa maeneo ya wazi na michezo mimi nitasimia na kuhakikisha yanatunzwa’ alisema Byakanwa.
Mradi wa Ujenzi wa Bustani za kupumzikia za Tilla, Maduka Makubwa na Mashujaa ulianza mwezi Juni, 2018 ukigharimu fedha cha shilingi Bilioni 1.4. Mradi huu umetekelezwa na Manispaa ya Mtwara-Mikindani kupitia Mradi wa Uendelezaji Miji Mkakati(TSCP).
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.