Halmashauri chini ya idara ya Maji ina jukumu la kutoa huduma ya maji safi na salama hususani ya visima kwenye kata za pembezoni mwa Manispaa.
Idadi ya wakazi wapatao maji safi na salama ni 88,534 kati ya 124,697 sawa na asilimia 71, na jumla ya wakazi wapatao maji safi na salama pembezoni mwa Manispaa ni 14,940 kati ya 18,824 sawa na asilimia 80.4 waliobaki sawa na asilimia 19.6 wanatumia vyanzo vya maji asili.
MAJUKUMU YA MSINGI YA IDARA YA MAJI
SHUGHULI ZILIZOFANYIKA
1.Uchimbaji wa visima 11 virefu pembezoni mwa manispaa umefanyika.
2.Miradi 6 ya mfumo wa maji ya bomba maeneo ya Mjimwema, Mkangala, Rwelu, Haikata, Minyembe na Mbae imejengwa.
3.Visima 22 vifupi vilivyofungwa pampu za mkono vimekarabatiwa
4.Jumla ya vyombo 5 vya watumiaji maji vimeundwa na kupewa mafunzo juu ya uendeshaji wa miradi ya maji.
HALI YA UPATIKANAJI WA HUDUMA YA MAJI
Halmashauri inatekeleza miradi ya maji ya vijiji kumi kupitia Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Maji (WSDP) . Program hii inafadhiliwa na wahisani mbalimbali wa Maendeleo kama World Bank, ADfB, Serikali ya Ujerumani na Ufaransa n.k. Pia utekelezaji wa Miradi ya maji ya vijiji kumi umeingizwa kwenye mpango wa Big Result Now (BRN).
Hadi sasa Halmashauri ina jumla ya Visima 39 kati ya hivyo visima virefu ni 8,vinavyofanya kazi ni visima 5. Visima vifupi ni 36, vinavyofanya kazi ni 21 na vibovu ni 15.
Kupitia Programu ya Sekta ya Maji imetekeleza miradi ya Maji (7) Saba kama ifuatavyo:-
1. Mradi wa maji Mji Mwema
Mradi huo umekamilikamita kwa asilimia 100, utekelezaji uliofanyika ni Ujenzi wa mfumo wa Maji ya bomba mita 3,021 , Ujenzi wa nyumba ya Mitambo, Ujenzi wa Tanki la maji lita 10,000 na mifumo 3 ya uvunaji wa maji ya mvua.
2. Mradi wa Maji Rwelu
Mradi huo umekamilika kwa asilimia 100, utekelezaji uliofanyika ni ujenzi wa mfumo wa Maji ya bomba mita 7,011 , Vituo 6 vya kuchotea Maji, Ujenzi wa nyumba ya Mitambo, Ujenzi wa Tanki la maji lita 50,000 na mifumo 3 ya uvunaji wa maji ya mvua.
3. Mradi wa Maji Mbae
Mradi huo umekamilika kwa asilimia 100, utekelezaji uliofanyika ni ujenzi wa mfumo wa Maji ya bomba mita 5,159 , Vituo 6 vya kuchotea Maji, Ujenzi wa nyumba ya Mitambo, Ujenzi wa Tanki la maji lita 50,000 na mifumo 3 ya uvunaji wa maji ya mvua.
4. Mradi wa Maji Mkangala
Mradi huo umekamilika kwa asilimia 100, utekelezaji uliofanyika ni ujenzi wa mfumo wa Maji ya bomba mita 11,843 , Vituo 8 vya kuchotea Maji, Ujenzi wa nyumba ya Mitambo, Ujenzi wa Tanki la maji lita 50,000 na mifumo 3 ya uvunaji wa maji ya mvua.
5. Mradi wa Maji Haikata
Mradi huo umekamilika kwa asilimia 100, utekelezaji uliofanyika ni ujenzi wa mfumo wa Maji ya bomba mita 2,041, Vituo 5 vya kuchotea Maji, Ujenzi wa nyumba ya Mitambo , Ujenzi wa Tanki la maji lita 25,000 na mifumo 3 ya uvunaji wa maji ya mvua.
6. Mradi wa Maji Minyembe
Mradi huo umekamilika kwa asilimia 100, utekelezaji uliofanyika ni ujenzi wa mfumo wa Maji ya bomba mita 5,409 , Vituo 5 vya kuchotea Maji, Ujenzi wa nyumba ya Mitambo, Ujenzi wa Tank la maji lita 75,000 na mifumo 3 ya uvunaji wa maji ya mvua.
7. Mradi wa Maji Mtawanya
Mradi huo umekamilika kwa asilimia 100, utekelezaji uliofanyika ni ujenzi wa mfumo wa Maji ya bomba mita 6,437 , Vituo 12 vya kuchotea Maji, Ujenzi wa nyumba ya Mitambo , Ujenzi wa Tank la maji lita 50,000 na mifumo 3 ya uvunaji wa maji ya mvua.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.