Majukumu ya kiengo cha Teknologia ya habari na mawasiliano.
Kutayarisha mpango Mkakati wa kuhusu Teknolojia ya habari na Mawasiliano, Miongozo na taratibu kwa kuzingatia Sera ya Taifa ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano.
Kuishauri Menejimenti ya Sekretarieti ya Halmashauri juu ya masuala yanayohusiana na sera zinazohusiana na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano na utekelezaji wa dhana ya serikali mtandao.
Kusimamia maendeleo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano na utekelezaji wake kwa ajili ya Sekretarieti ya Halmashauri ya Wilaya.
Kushirikiana na ORM-TAMISEMI kuratibu na kuendeleza viwango vya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano kwa ajili ya “software na hardware” kwa matumizi ya Sekretarieti ya Halmashauri na Mamlaka za Miji Midogo.
Kuziwezesha Mamlaka za Miji Midogo, Kata na vijiji katika kuendeleza na kutekeleza mipango/miradi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano.
Kuratibu utekelezaji wa usanifu na kutunza/kuiendeleza matumizi yanayohusiana na Tovuti na utunzaji wa kumbukumbu kwa ajili ya Halmashauri ya Wilaya, wizarani na wadau wengine.
Kutathimini, kuboresha na kusimamia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano na usimamizi wa mifumo ya taarifa/habari iliyosimikwa/iliyowekwa kwenye Halmashauri.
Kufanya tathimini ya mahitaji ya mafunzo juu ya usimamizi wa mifumo ya taarifa na teknolojia ya habari na mawasiliano na kuandaa mpango wa kujenga uwezo kwa watumishi wa Kitengo cha Tehama.
Kufanya tathimini ya hatari/hasara zinazohusiana na Miundombinu ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano na mfumo wa usimamizi wa taarifa na namna ya kuthibiti.
Kuendeleza na kutunza Tovuti ya Halmashauri.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.