Mtwara-Mikindani ni jina ambalo linamuunganiko wa maneno mawili ambayo ni Mtwara na Mikindani.. Sehemu hizi mbili yaani Mtwara na Mikindani vilikuwa ni vituo maarufu ambapo kila kimoja kilitokana na sababu zake .Neno ”Ntwara” ambalo kwa sasa Mtwara ni neno la Kimakonde lenye maana ya ku-twaaliwa (kuvamiwa na kuchukuliwa mateka). Baadae eneo hili likawa makazi ya Waarabu na watu wengine ambao waliyokuwa wametekwa kama Watumwa na kuuzwa.
Neno Mikindani limetokana na neno Mikinda yaani eneo ambalo miti ya minazi haikui/kustawi vizuri.Wanyeji halisi wa eneo hili ni Wamakonde,Wayao na Wamakua. Asilimia 75 ya wananchi wa Mtwara ni Wamakonde,wafuatiwa na Wayao na mwisho ni Wamakua. Kama kawaida ya Mikoa mingine ya Tanzania kuna watu wengine wanaichi Mtwara.
Historia ya kuanzishwa mamlaka kamili ya Halmashauri ya Mtwara-Mikindani Manispaa yalianza mwaka 1948, kipindi cha utawala wa kikoloni wanaamisha Bandari ya Mtwara kutoka Mikindani ambapo ilipokuwa awali.
Manispaa ya Mtwara Mikindani ina ukubwa wa kilometa za mraba 163 sawa na 0.97% ya eneo lote la Mkoa wa Mtwara. Manispaa ya Mtwara Mikindani kwa upande wa mashariki imepakana na bahari ya hindi, upande wa kaskazini, upande wa magharibi na upande wa kusini imepakana na halmashauri ya wilaya ya Mtwara. Halmashauri hii kiutawala imegawanyika katika maeneo yafuatayo ina Jimbo moja la uchaguzi, Kata 18,Mitaa 111 na Tarafa 2.
Kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2012, idadi ya watu Manispaa ilikuwa 108,299 (Ke 57,237 na Me 51,062) Hadi Kufikia 2017 halmashauri inakadiriwa kuwa na watu 115,623 kwa ongezeko la 1.6% kwa mwaka (Ke 61,108, na Me 54,515).
Kwa upande wa shughuli za kiuchumi, asilimia 84 ya wananchi wa Manispaa ya Mtwara Mikindani wanajishughulisha na biashara, asilimia 12.4 wanajishughulisha na kilimo, ambapo mazao ya chakula ni Mahindi, Muhogo, Mtama, Mbaazi, Njugu mawe, Kunde. Mazao ya biashara yanayolimwa ni Korosho, Karanga na Ufuta na asilimia 3.6 ya wananchi wa Manispaa wanajishughulisha na viwanda vidogo vidogo na vya kati.
Halmashauri imetenga na kupima viwanja vyenye ukubwa wa ekari 505.47 kwa ajili ya ujenzi wa viwanda, maghala na kituo kikubwa cha umeme. Viwanja hivi vimepimwa katika maeneo ya Mtepwezi katika kata ya Likombe na maeneo ya Chihiko katika kata ya Mtawanya. Mpaka sasa, halmashauri ina jumla ya ekari 281.62 yenye viwanja 74 ambavyo vipo tayari kwa ajili ya waombaji mbalimbali walio tayari kujenga viwanda. Pamoja na kutenga maeneo kwa ajili ya viwanda, Halmashauri imepima pia eneo lenye ukubwa wa ekari 223.85 kwa ajili ya kujenga kituo cha umeme katika eneo la Mtepwezi. .
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.