MAJUKUMU YA KITENGO CHA USIMAMZI WA MANUNUZI
- Kusimamia manunuzi yote na uuzaji wa mali chakavu kwa zabuni kwenye taasisi isipokuwa kutolea maamuzi ya kisheria na tuzo za mikataba.
- Kuwezesha kazi za zabuni.
- Kutekeleza maamuzi ya bodi ya zabuni.
- Kuandaa mpango wa manunuzi na uuzaji wa mali chakavu kwa taratibu za zabuni.
- Kupendekeza manunuzi na uuzaji wa mali chakavu kwa taratibu za zabuni.
- Kuangalia na kuandaa maelezo ya mahitaji.
- Kuandaa makabrasha ya zabuni.
- Kuandaa matangazo ya zabuni.
- Kuandaa makabrasha ya zabuni..
- Kutoa makabrasha ya mikataba iliyothibitishwa.
- Kutunza kumbukumbu za manunuzi na michakato ya uuzaji wa mali chakavu.
- Kutunza orodha au rejesta ya mikataba yote.
- Kuandaa taarifa ya mwezi kwa bodi ya zabuni.
- Kuandaa na kuwasilisha kwenye vikao vya menejimenti taarifa ya robo ya utekelezaji wa mpango wa manunuzi.
- Kuunganisha manunuzi na uuzaji wa mali chakavu ya Idara zote za taasisi.
- Kutayarisha taarifa zingine zitakazohitajika.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.