Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Abdallah Mwaipaya amevitaka vikundi 58 vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu vilivyokidhi vigezo na kupata mkopo wa asilimia kumi usiokuwa na riba shilingi 640,985,000 kutoka Manispaa ya Mtwara-Mikindani kuhakikisha wanafanya marejesho kwa hiyari ili vikundi vingine viweze kunufaika na mikopo hiyo.
“Mikopo hii si zawadi, mikopo hii sio sadaka, hakikisheni mkishapokea fedha mnafanya shughuli mlizozipambanua na mufanye marejesho kwa wakati sahihi bila kushurutishwa ili muweze kupata mikopo tena mkishamaliza”amesema Mhe. Mwaipaya
Ametoa rai hiyo Leo Januari 6,2025 alipohudhuria kwenye hafla ya kukabidhi hundi ya mfano ya mikopo kwa vikundi 58 vya Wanawake , Vijana na watu wenye ulemavu iliyofanyika katika Ukumbi wa Bustani ya Tilla.
Mhe. Mwaipaya amemuelekeza Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani Mwalimu Hassan Nyange kuhakikisha anavikopesha tena vikundi vitakavyokamilisha ulipaji wa marejesho kwa wakati huku akiwaasa vikundi vya vijana na watu wenye ulemavu kuchangamkia fursa ya kukopa mikopo ya halmashauri isiyokuwa na riba ili waweze kujiajiri.
Aidha amempongeza Mkurugenzi kwa kuwa halmashauri ya kwanza katika Wilaya yake kutoa mikopo hiyo na ametoa agizo kwa halmashauri nyingine kuhakikisha wanakopesha mara moja.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Mtwara Mjini Mhe. Hassan Mtenga amewasisitiza wajasiriamali hao kufanya marejesho kwa wakati na kuzitumia fedha hizo kwa kazi walioikusudia ili iweze kuwaletea tija kwa sababu mkopo hu oni wa kukopa na kulipa.
Nae Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Mtwara Mjini Mhe. Salumu Naida Ameipongeza Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mtwara na Mkurugenzi kwa kuwezesha vikundi vya wajasiriamali kiuchumi kwa kuwapatia mkopo usiokuwa na riba kwani inawapunguzia adha ya kuingia mikopo mingine yenye dhamana isiyofaa na kausha damu.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.