MAJUKUMU YA KITENGO CHA SHERIA KATIKA HALMASHAURI.
1. Kusimamia uendeshaji wa jumla wa Halmashauri , kuhakikisha sheria , kanuni, taratibu,miongozo mbalimbali ya serikali
inazingatiwa katika uendeshaji wa jumla wa Halmashauri.
2. Kusimamia na kushauri uendeshaji wa jumla wa vikao vya menejimenti, kamati za kudumu za robo mwaka na mikutano ya baraza kufuata kanuni za uendeshaji wa mikutano zilizopo pamoja na miongozo mbalimbali inayotolewa na serikali.
3. Kusimamia masuala yote ya kisheria yahusuyo mashauri mbalimbali na mienendo ya kesi za Halmashauri katika vyombo vyote
vya kisheria zikiwemo mahakama ngazi zote (Rufaa, Kuu, Mkoa na Wilaya) na mabaraza yote (Ardhi na Nyumba,Usululisho na Uamuzi n.k).
4. Kusimamia mchakato wa maandalizi ya utungaji na au uhuishaji wa mara kwa mara wa rasimu za sheria ndogo za Halmashauri zilizobadilika kisera au kupitwa na wakati.
5. Kusimamia utekerezaji wa sheria ndogo zilizotungwa katika utekelezaji wa majukumu ya Halmashauri wa kila siku.
6. Kutoa tafsiri ya sheria mbalimbali na elimu ya jumla kwa Umma na Watumishi kuhusu sheria-mama za Nchi na sheria ndogo.
7. Kuyasimamia na kuratibu uendeshaji wa mabaraza ya kata katika Halmashauri.
8. Kushauri taratibu za manunuzi na kufanya ukaguzi wa mikataba yote ya Halmashauri kabla ya kusainiwa.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.