• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mtwara Mikindani Municipal Council
Mtwara Mikindani Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Manispaa ya Mtwara Mikindani

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Idara
      • Elimu ya Sekondari
      • Elimu ya Msingi
      • Idara ya Maji
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na biashara
      • Afya
      • Usafi na Mazingira
      • Ujenzi
      • Mipango Miji, Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ufugaji na Uvuvi
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
    • Kitengo
      • Ukaguzi wa ndani
      • Teknolojia, Habari, Mawasiliano na Mahusiano
      • Manunuzi na Ugavi
        • Fursa za Uwekezaji
          • Vivutio vya Utalii
          • Maeneo ya Viwanda
      • Ufugaji wa nyuki
      • Uchaguzi
      • Sheria
    • Muundo wa Kiutawala
    • Kata
      • Shangani
      • Rahaleo
      • Reli
      • Vigaeni
      • Majengo
      • Magomeni
      • Ufukoni
      • Mitengo
      • Magengeni
      • Mtonya
      • Kisungule
      • Jangwani
      • Mtawanya
      • Naliendele
      • Chikongola
      • Chuno
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Maeneo ya Viwanda
  • Huduma
    • huduma za maji
    • Huduma za afya
    • Huduma za elimu
    • HUduma za watumishi
    • Uzoaji wa taka ngumu
  • Madiwani
    • Orodha ya Wahe. Wabunge na Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipangomiji na Ujenzi
      • Huduma za Jamii
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Ratiba za Vikao
      • Kumuona Mstahiki Meya
  • Mradi
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi mipya
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Miongozo
    • Fomu
    • Huduma kwa Mteja
    • Ripoti
    • Mpango Mkakati
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Videos
    • Hotuba
    • Maktaba cha Picha

Fedha na Uongozi

Kamati ya Fedha na Uongozi:

 

Majukumu ya jumla:

Kamati hii inawashirikisha Wenyeviti wa Kamati zote za kudumu na inapaswa kukutana kila mwezi mara moja. Aidha, madaraka ya Kamati hii ni kama ya Kamati zingine za kudumu na hivyo hairuhusiwi kisheria kufanya kazi/majukumu ya Kamati zingine za kudumu. Kwa ujumla, majukumu yake ni pamoja na kusimamia na kudhibiti ukusanyaji wa mapato na matumizi ya mali ya Halmashauri kwa kupitia vikao vyake.

Majukumu Maalum ya Kamati:

  • Kuweka mikakati na kupendekeza uongezaji wa mapato
  • Kuwasilisha mapendekezo ya Bajeti na mpango wa Maendeleo kwenye Halmashauri ili kuidhinishwa na Halmashauri.
  • Kusimamia utunzaji wa hesabu za fedha ikiwa ni pamoja na uhakiki wa mali za Halmashauri, ukusanyaji wa mapato, kufuta madeni, na kuomba vibali maalum kwa matumizi yanayohitaji kibali cha Waziri mwenye dhamana ya Serikali za Mitaa.
  • Kufikiria na, inapowezekana, kupendekeza kwenye Halmashauri masuala yanayohusu Sheria Ndogo na utendaji katika ngazi za chini za Halmashauri.
  • Kupokea na kuzingatia mapendekezo ya kubadili matumizi ya mafungu ya fedha (re-allocation) yaliyopo katika makisio yaliyoidhinishwa na kuyapeleka kwa Halmashauri.
  • Kuratibu mapendekezo kutoka kwenye Kamati zingine kuhusu matumizi ya kawaida na miradi na kuyawasilisha kwenye Halmashauri.
  • Kufikiria na kupendekeza kwenye Halmashauri mikopo yote ya Halmashauri.
  • Kutoa mapendekezo ya vitega uchumi kwa madhumuni ya kuongeza mapato kwa mujibu wa Sheria ya Fedha za Serikali za Mitaa, Sura ya 290.
  • Kupokea na kujadili taarifa za wakaguzi wa fedha na mali ya Halmashauri na kupendekeza hatua za kuchukuliwa kutokana na maelekezo na maoni ya wakaguzi kwa mujibu wa Sheria za Serikali za Mitaa, Sura ya 290.
  • Kusimamia na kudhibiti matumizi ya fedha za Halmashauri, kwa kuzingatia taratibu zilizowekwa na Waziri na taratibu nyingine zitakazowekwa na Halmashauri;
  • Kupitia marekebisho yote yaliyopendekezwa hususan kuhusu taratibu za fedha, ikiwa ni pamoja na mapitio ya mara kwa mara yanayohusu thamani ya fedha ambapo Kanuni mbalimbali za manunuzi ya mali na vifaa hutumika;
  • Kufikiria na kupendekeza mabadiliko ya viwango vya kodi, ada na ushuru mbalimbali, vinavyotolewa na Halmashauri;
  • Kufikiria mapendekezo ya Bajeti na Mipango ya Maendeleo ya kila Kamati ya Kudumu na kuiwasilisha kwenye Halmashauri ili kupata idhini;
  • Kushughulikia tofauti ya mapato na matumizi katika bajeti yote na kupendekeza hatua stahiki ya kuchukua kuondoa mapungufu katika mapato au ziada ya matumizi;
  • Kufikiria mapendekezo yote yanayohusu matumizi makubwa ya fedha kabla hayajawasilishwa kwenye Halmashauri ili kupata idhini;
  • Kupokea mahesabu ya mwaka ya Halmashauri na kuhakikisha taarifa ya mahesabu ya mwaka inawasilishwa kwa wakati kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali;
  • Kupitia na kuidhinisha mpango wa manunuzi wa Halmashauri kwa kuzingatia mpango wa Bajeti uliopitishwa na Halmashauri;
  • Kupitia taarifa ya kila robo mwaka kuhusu Manunuzi iliyowasilishwa na Afisa Masuuli;
  • Kusimamia utekelezaji wa mikataba ya Halmashauri kwa kukagua miradi inayotekelezwa na vifaa vilivyopokelewa;
  • Kumwelekeza Mkurugenzi kufanya manunuzi au ukaguzi wa huduma au vifaa vilivyonunuliwa ili kupata thamani halisi, itafanyika hivyo endapo itadhihirika kwamba, maelezo yaliyotolewa kuhusu manunuzi ya vifaa au huduma hayaridhishi;
  • Kuidhinisha majina ya wajumbe wa Bodi ya zabuni na wa Bodi zingine kwa mujibu wa Sheria husika;
  • Kushughulikia orodha ya wadaiwa wote itakayokayowasilishwa kwenye Kamati na kutoa mapendekezo ya hatua za kuchukua;
  • Kupendekeza njia na taratibu za kuondosha vifaa chakavu. Uondoshaji wa vifaa unaweza kufanyika kwa njia ya kuuza au kuviharibu;
  • Kujadili na kupitia taarifa za fedha za kila mwezi na kila robo mwaka;
  • Kupendekeza kwa Halmashauri hatua za kuchukua kuhusu kufuta madeni ya Halmashauri;
  • Kushughulikia Sera kuhusu kukopa na uwekezaji,
  • Kubuni na kupendekeza mpango wa kuanzisha na kuendeleza uhusiano na Halmashauri nyingine.
  • Kurekebisha na kusimamia makusanyo na matumizi ya mapato ya vijiji / mitaa na kata kwa mujibu wa Sheria,  
  • Kuteua wakaguzi wa fedha/mali za Serikali za Vijiji kwa mujibu wa Sheria, Sura ya 290).
  • Kujadili na kutoa mapendekezo ya hatua za kuchukuliwa kuhusu mambo yote yanayohusu masuala ya ajira na nidhamu ya wafanyakazi na watumishi.
  • Kujadili na kutoa mapendekezo kuhusu masuala yanayohusu nyumba za Halmashauri.
  • Kupokea na kutoa uamuzi juu ya mapendekezo ya watumishi wanaokwenda masomoni.
  • Kujadili na kupendekeza masuala yote yanayohusu maslahi ya jumla ya watumishi, ikiwa ni pamoja na mikopo, nyumba, usafiri, matibabu, rambirambi na motisha nyinginezo.
  • Kupitisha mapendekezo ya kuthibitisha watumishi kazini baada ya kumaliza kipindi cha majaribio kulingana na miundo husika ya utumishi.

Matangazo

  • Taarifa Kwa Umma ya Ilani ya Kuondoka Kwenye Kiwanja Nmaba 1-149 Litingi January 03, 2025
  • Taarifa Kwa Umma Ufafanuzi Kuhusu Jina la Shule ya Sekondari Mwalimu Nyange January 02, 2025
  • Terms Of Reference For The Provisions Of Construction Supervision Consultancy Services For Urban Infrastructures Development In Mtwara Mikindani Municipality Under The TACTIC Project March 07, 2025
  • Tangazo la Kuitwa Kwenye Usaili Nafasi ya Mwandikishaji Msaidizi na BVR Operators January 09, 2025
  • Tazama yote

Habari mpya

  • Kamati ya Siasa Mkoa Yapongeza Utekeelzaji wa Miradi ya MaendeleoMtwara-Mikindani

    January 08, 2025
  • MD Nyange Ateta na Watumishi Wa Kada ya Afya

    January 07, 2025
  • Vikundi Vilivyopata Mkopo Vyahimizwa Kurejesha Fedha Kwa Wakati

    January 06, 2025
  • Mtwara-Mikindani Yatoa Mkopo wa Mil.640.9 Kwa Vikundi 58

    January 06, 2025
  • Tazama yote

Video

Namna ya Kujisajili na Kutumia mfumo wa Uhamisho kwa watumishi wa Umma
Video nyinginezo

Viunganishi vya haraka

  • Zabuni ya ujenzi wa barabara km 4.1,Ujenzi wa Mfereji wa maji ya mvua toka Skoya,nabwada hadi Mtepwezi,Ujenzi wa soko la Chuno,Ukarabati wa stendi ya Mikindani pamoja na Uboreshaji wa sehemu za kupumzikia na michezo
  • Kupata matokeo ya Darasa la nne 2017 Manispaa Mtwara-Mikindani
  • Matokeo ya Kidato cha Pili 2017 Manispaa Mtwara-Mikindani
  • Taratibu za Kupata fomu za Vileo

Viunganishi linganifu

  • Tovuti kuu ya Serikali
  • OR - TAMISEMI
  • Wakala ya Serikali Mtandao
  • Utumishi wa Umma
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Takwimu ya Taifa

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    Manispaa Mtwara-Mikindani

    Anuani ya Posta: P. o. Box 92,

    Simu ya mezani: 023-2333102

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.