Mnamo mwezi November 2013 TASAF awamu ya tatu ilianza kutekelezwa kwa kuainisha kaya masikini sana,jumla ya kaya 1,321 zilitambuliwa na tayari zimeanza kunufaika na Mpango wa kunusuru Kaya Maskini(PSSN). TASAF III itatekelezwa kwa miaka kumi katika Awamu mbili za miaka mitano kila Awamu kaya. Mpango wa TASAF III una sehemu kuu nne za utekelezaji, ambazo ni :-
Mpango wa kunusuru kaya maskini, ambao unatoa ruzuku kwa kaya maskini sana hususan zenye wajawazito na watoto ili ziweze kupata huduma za elimu na afya. Pia kutoa ajira kwa kaya maskini zenye watu wenye uwezo wa kufanya kazi wakati wa majanga mbalimbali kwa mfano ukame, mafuriko n.k.
1.1 LENGO kuu la TASAF III ni kuziwezesha kaya maskini sana kuongeza kipato,fursa na uweza wa kujiletea maendeleo na kuongeza matumizi muhimu kaya.
1.2 MADHUMUNI YA MPANGO (TASAF III)
1.3 VIGEZO VINAVYOTUMIKA KUTAMBUA KAYA MASKINI SANA
MIRADI YA AJIRA YA MUDA (PUBLIC WORKS PROGRAM-PWP)
Manispaa ya Mtwara Mikindani kwa mwaka 2014/2015 na mwaka 2016/17 imetekeleza miradi ya ajira ya muda kwa mitaa 35 ikijumuisha miradi mbalimbali ya ujenzi na mazingira,ambayo iliwezesha walengwa 1290 kujiongezea kipato.
MADHUMUNI YA MIRADI YA MUDA
MIRADI YA UJENZI WA MIUNDO MBINU YA JAMII
Manispaa ya Mtwara- Mikindani kupitia utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa miundombinu ya jamii imetekeleza mradi wa kujenga Nyumba ya Mganga katika Mtaa wa Rwelu (Zahanati ya Lwelu) ambayo iligharimu kiasi cha Tsh.66,180,500.00.
MADHUMUNI YA MIRADI YA MIUNDO MBINU
MIRADI YA KUWEKA AKIBA NA KUWEKEZA
Manispaa ya Mtwara Mikindani ina jumla ya ya vikundi 76 vya kuweka akiba na kuwekeza kwa walengwa wote waliopo katika mpango ambapo kila kikundi kina walengwa 10 hadi 15 na mpaka sasa kuna Vikundi 33 vimeanza kuweka Akiba na kuwekeza katika miradi midogo midogo ambayo kwa sasa wameweza kukusanya TSH 9,124,000.00.
Lengo kuu ni la walengwa kujiunga vikundi vya kuweka Akiba ni kukuza utamaduni wa kujiwekea akiba kwa kaya maskini ili kuwawezesha kukabiliana na dharura na mahitaji ya msingi
MALENGO KUHAMASISHA KAYA KUWEKA AKIBA NA KUWEKEZA
UKELEZAJI WA SHUGHULI CHA MRADI CHA TASAF
Mradi unatekeleza majukumu yake kwa kushirikiana na idara zote katika halmashauri kwa kutegemea aina miradi iliyoibuliwa,kusanifiwa na inayotekezwa(Uratibu kisekta), vile vile kwa kuzingatia umuhimu wa TEHAMA Mfumo wa compyuta ndio hutumika kuingiza taarifa za kaya,kuandaa mchakato wote wa malipo na nyaraka zote zinahitajika wakati wa zoezi la malipo, kushughulikia malalamiko na madai ya walengwa pale yanapojitokeza.
MAFANIKIO YALIYOFIKIWA HALMASHAURI KUPITIA TASAF
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.