Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Dunstan Kyobya Agosti 22,2020 amezindua rasmi siku ya wanafamilia wa Kituo cha afya Likombe (Likombe Family Day) na kuwapongeza watumishi hao kwa kuandaa siku hiyo muhimu.
"Ni Taasisi chache zenye majukumu mengi kama yenu ambao wananweza kuandaa kitu kama hiki hongereni sana " alisema Kyobya
Aidha amezitaka Taasisi nyingine kuiga Mambo mazuri yanayofanywa na Kituo hiki ikiwemo Uanzishwaji wa siku ya wanafamilia .
Pamoja na Uzinduzi huo Kyobya alitembelea wodi ya akina mama wajawazito na watoto kwa lengo la kuwasalimia na kuwapa zawadi ikiwa ni sehemu ya kuwafariji
Kwa upande wake Mganga Mfawidhi wa Kituo hiko Dkt. Nuru Namkuna amesema kuwa lengo la kuanzishwa kwa siku ya wanafamilia wa Kituo cha afya Likombe ni pamoja na kujenga mahusiano baina ya watumishi , jamii na wadau mbalimbali wa afya pamoja na kuburudika ili kuleta ufanisi katika kazi.
Uzinduzi wa siku ya wanafamilia ulitanguliwa na shughuli nyingi zikziwemo Uchangishaji wa damu salama ambapo jumla ya chupa 131 zilikusanywa pamoja na upimaji wa saratani ya shingo ya kizazi kwa akina mama wapatao 49.
Siku ya wanafamilia wa Likombe imezinduliwa rasmi Agosti 22,2020 na inatarajia kufanyika kila mwaka.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.