UNWOMEN YATOA ELIMU YA UMILIKI WA PAMOJA WA MAPATO YATOKANAYO NA KILIMO KATA YA JANGWANI
Shirika la umoja wa kimataifa la wanawake (UNWOMEN) kupitia mradi wa wanawake Uongozi na Haki ya kiuchumi (WLer) Machi 22,2024 wametoa elimu ya kuhusu uhamasishaji wa haki za wanawake katika usawa wa umiliki wa pamoja wa mapato yatokanayo na kilimo katika Kata ya Jangwani Mtaa wa Mahuta.
Afisa Maendeleo ya Jamii wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani Bi Rida Kahungenge ambae pia ni mratibu wa Mradi huo amesema kuwa lengo la elimu hiyo ni kuitaka jamii kuwa na dhana shirikishi ya kuwa na uchumi wa pamoja.
Aidha ametoa rai kwa jamii hadi ngazi ya familia kuwa na akaunti ya pamoja ikiwa ni utaratibu wa kulinda haki za wanawake kiuchumi.
Reniuce Mhagama ni mhandisi Kilimo ambae pia ni mwezeshaji katika mradi huo alisema kuwa kukosekana kwa usawa kunarudisha nyuma maendeleo katika familia na kuongeza kuwa ni wakati wa familia kushirikishana katika kupanga malengo na mikakati ya pamoja kuanzia katika uzalishaji hadi inapofikia hatua ya matumizi,
Katika Manispaa ya Mtwara-Mikindani Mradi huo unatekelezwa katika Kata tatu ambazo ni Kata ya Chuno mtaa wa Majengo na Ligula B.Kata ya Naliendele Mtaa wa Pwani B na Naulongo pamoja na Kata ya Jangwani Mtaa wa Mahut ana Lwelu
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.