MTWARA-MIKINDANI KULIPA WALIMU WA KUJITOLEA WA MICHEPUO YA SAYANSI
Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani Mwalimu Hassan B.Nyange Amesema kuwa kutokana na Upungufu wa Walimu wa Masomo ya Sayansi katika Shule za Sekondari Kuanzia April 1,2024 Atalipa kiasi cha Shilingi Milioni moja,laki mbili (1,200,000) kwa walimu wa kujitolea wanne wa masomo ya Sayansi kwa Shule ya Sekondari ya Mkanaredi,Naliendele,Mangamba na Likombe kupitia Makusanyo ya mapato ya ndani ambapo kila mmoja atalipwa Shilingi laki tatu (300,000) ili kuongeza motisha kwa walimu katika ufundishaji.
Akizungumza Katika kikao kilichowakutanisha Watendaji Kata,Mitaa,Maafisa Elimu,Wakuu wa Shule za Serikali na Binafsi na Walimu Wakuu kilichofanyika Machi 19,2024 katika Shule ya Sekondari ya Mtwara Ufundi Nyange Alisema kuwa anaendelea kutatua changamoto za walimu ikiwemo kulipa madai ya likizo na uhamisho ili waweze kusimamia vyema taaluma kwenye shule wanazofundisha.
Aidha alisema kuanzia aprili 1,2024 ataunda kamati kutoka kwenye ofisi yake itayohoji wanafunzi wanafunzi kuhusiana na walimu wanaojihusisha kimapenzi na mwanafunzi au kumpa mimba na mara watakapobainika watachuliwa hatua kali za kisheria
Nae Mkuu wa Dawati la jinsia na Watoto A/INSP Juliana Chenge aliwaasa viongozi hao kuzingatia viapo na maadili ya kazi zao kwa kutojihusisha na vitendo vya ukatili kwa Watoto badala yake watoe elimu kwa jamii na kuwataka walimu kuanzisha Madawati ya jinsia kwenye shule zao ziweze kuwasaidia wanafunzi kuwasilisha changamoto zao,
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.