Kaimu Mkurugenzi wa Mnispaa ya Mtwara-Mikindani Dkt Joseph Kisala amewataka wananchi wa Kata ya Majengo kulinda Miundombinu rafiki inayojengwa na Serikali ikiwemo mradi wa Taa mpya zinazowekwa pembezoni mwa Barabara ili kupendezesha mji wetu.
Hayo yamesemwa leo Machi 22,2024 katika mkutano na wananchi wa Majengo wa kusikiliza na kutatua kero uliofanyika katika viwanja vya Ofisi ya Kata ya Majengo,
Alisema kuwa licha ya Serikali kutumia fedha nyingi katika kuimarisha miradi ya maendelo bado kuna watu wanaishi katika jamii zetu wanahujumu miundombinu hiyo kwa kuiba vifaa mbalimbali kama vile nyaya za taa ambapo wanarudisha nyuma maendeleo ya wanamtwara.
Aidha ametoa wito kwa jamii kuwa na wivu wa maendeleo kwa kuwafichua waharifu hao,wakiti huohuo kutokana na uwepo wa ajali za mara kwa mara wananchi hao wamemuonesha na kumuomba Kaimu Mkurugenzi kuifanyia kazi kero ya kona kali ya barabara ya (Kilimanjaro) inayotoka Soko kuu hadi LIkombe.
Naye Diwani wa Kata ya Majengo Mhe. Sixmund Lungu ambaye pia ni Naibu Meya wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani Alisema kuwa wananchi wake wana kero nyingi lakini zile za msingi zinatakiwa kutekelezwa kwa haraka na kwa wakati kama vile maji na umeme.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.