Mkuu w aWilaya ya Mtwara Mhe.Evod Mmanda akikabidhi pikipiki kwa Afisa Mtendaji wa Kata ya Ufukoni Bi Philomena Mwangwale,zoezi la makabidhiano limefanyika April 17,2019 katika viwanja vya Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa
Katika kuteleza ilani ya Chama cha Mapinduzi ibara ya 16 inayosisitiza suala la kufanya kazi kwa bidii na kwa weledi ili kuongeza mapato, Manispaa ya Mtwara-Mikindani imetumia shilingi milioni 11.5 katika ununuzi wa pikipiki tano na kuzigawa kwa watumishi wa Idara ya Utawala na Fedha.
Akizungumza wakati wa ugawaji wa pikipiki hizo ulifaonyika April17,2019 katika Viwanja vya Ofisi za Manispaa, Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Evod Mmanda ameipongeza Manispaa ya Mtwara-Mikindani kwa uamuzi wa kununua pikipiki hizo kwa kutumia mapato ya ndani na kuzigawa kwa watumishi wa Idara hizo kwa kuwa kila idara ni muhimu katika kufanikisha maendeleo ya Manispaa.
Pamoja na pongezi hizo Mmanda amewataka waliokabidhiwa pikipiki kuzitumia katika kufanya kazi za Serikali zitakazoleta matokeo chanya badala ya kuzigeuza bodaboda na kufanya shughuli za binafsi hasa nyakati za usiku na kwenye sehmu za starehe.
Aidha amewataka watumishi hao kuzingatia sheria za barabarani kwa sababu ni fedheha ukikamatwa ukiwa una makosa na kuwataka wasio kuwa na sifa za udereva kukamilisha taratibu kabla hawajanza kuziendesha.
Awali akisoma taarifa ya ununuzi wa pikipiki hizo Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani kanali Emanuel Mwaigobeko amesema kuwa Manispaa imegawa pikipiki kwa watendaji hao kukiwa na malengo ya kuboresha na kuongeza mapato ya halmashauri, kurahisisha usambazaji wa taarifa kwa wakati pamoja na kurahisisha mifumo ya utoaji huduma kwa wananchi na kwa wakati.
Mwaigobeko amesema kuwa pamoja na pikipiki hizo kugawiwa kwa idara zingine Manispaa imedhamiria kuwapatia pikipiki watendaji wote wa Kata 18, hivyo pamoja na pikipiki 5 zilizogawiwa leo tayari katika bajeti iliyopita ilishanunua pikipiki 5 na kuzigawa kwa watendaji wa Kata 5 na hivyo kufanya jumla ya pikipiki zilizogaiwa kwa watendaji wa Kata kufikia 7.
Idara zilizopatiwa pikipiki ni pamoja na Idara ya Utawala (watendaji wa Kata wawili na Kitengo cha Masijala1) pamoja na Muhasibu wa mapato na Afisa TEHAMA. Aidha Katika bajeti ya 2019/2020 Manispaa imetenga jumla ya shilingi milioni…… ya ujunuzi wa pikipiki.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.