TANGAZO
HALMASHAURI YA MANISPAA YA MTWARA – MIKINDANI
UFANUNUZI WA MABADILIKO YANAYOTAKIWA YA MAJINA KWENYE AKAUNTI ZA MISHAHARA ZA WATUMISHI
1. Ni lazima majina MAWILI ya kaunti ya MSHAHARA yawe yanafanana na majina yaliyoko kwenye CHEKI NAMBA yako kwa mfano:
Kwenye Salary Slip Unaitwa: KOKOTO ZEGE HALILALI
Benki Unaitwa: KOKOTO HALILALI – Mshahara Utalipwa
Benki Unaitwa KOKOTO ZEGE Mshahara Utalipwa
Benki Unaitwa: ZEGE LIMECHACHA - Mshahara Haulipwi
2. Utofauti mdogo wa matamshi ya HERUFI au UANDISHI kwenye majina ya mtumishi kwenye AKAUNTI na CHEKI NAMBA hautaathiri malipo yake ya MSHAHARA kwa mfano:
Kwenye Salary Slip Unaitwa: KUMBILAMEDI YUSUPH Mshahara unalipwa
Benki Unaitwa: KUMBILAMEDI YUSUFU
3. Mpangilio wa majina ya mtumishi kwenye AKAUNTI YA BENKI na CHEKI NAMBA hautaathiri malipo yake ya Mshahara kama majina hayo yote yanafanana isipokuwa kwa mpangilio ndio tofauti kwa mfano:
KOKOTO ZEGE HALILALI
HALILALI ZEGE KOKOTO Mshahara utalipwa bila shida yoyote
ZEGE KOKOTO HALILALI
N.B. Unashauriwa kufanya uhakiki huu kwa kuangalia majina yaliyoko kwenye SALARY SLIP yako na majina yaliyoko BENKI kwa kuzingatia muongozo huu
Imetolewa na:
Idara ya Utawala na Utumishi
Mtwara – Mikindani
05/06/2017
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.