Katika kuhakikisha kuwa Mkakati wa Serikali wa uboreshaji wa Shule Kongwe zilizopo nchini unatekelezwa Manispaa ya Mtwara-Mikindani kupitia Shule ya Sekondari ya Wasichana Mtwara imepokea fedha shilingi Milioni 776,605,047.27 kutoka Serikali kuu kwa ajili ya ukarabati wa Miundombinu .
Fedha hizo zilizopokelewa Februari 5,2020 zinakwenda kutimiza ahadi ya Serikali ya awamu ya tano ya kuhakikisha inaboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia nchini.
Akizungumza Ofisini kwake Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani Col. Emanuel Mwaigobeko ameishukuru Serikali na kusema kuwa fedha zilizotolewa zitasaidia kwa kiasi kikubwa kuboresha miundombinu iliyochakaa katika shule hiyo.
Amesema kuwa Maandalizi ya awali kwa ajili ya ukarabati wa miundombinu hiyo yameshaanza na kwamba ujenzi utaanza hivi karibuni ukihusisha Madarasa, Mabweni , Ofisi pamoja na majengo mengine.
Shule ya Sekondari ya Wasichana Mtwara ni miongoni mwa shule kongwe zilizopo nchini Iliyonzishwa mwaka 1956 wakati huo ikijulikana kwa jina la Shule ya Wasichana Mtwara (Mtwara Girls School) na ilikuwa inatumika kama Shule ya Kati (Middle School) iliyokuwa inafundisha kuanzia darasa la nne hadi la Sita.
Mwaka 1961 Shule hii ilibadilishwa mfumo na kuwa Shule ya Sekondari ya Wasichana Mtwara (Mtwara Girls Secondary School) ikifundisha kuanzia kidato kwanza hadi cha nne, Aidha mwaka 1999 Shule hii pia ilianza kutoa Elimu ya Kidato cha Tano na Sita.
Maandalizi ya Ukarabati wa miundombinu hiyo yameshaanza ikiwemo ujenzi unaotarajia kuanza hivi karibuni Ukihusisha miundombonu ya madarasa, mabweni, Ofisi pamoja na majengo mengine yaliyopo .
Hii ni awamu ya pili kwa Manispaa ya Mtwara-Mikindani kupokea fedha kutoka Serikali kuu kukarabati Shule Kongwe ambapo awali ilipokea shilingi Bilioni 1,315,321,710 zilizotumika kukarabati Shule ya Sekondari ya Mtwara Ufundi ambapo ukarabati huo umeshakamilika.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.