Manispaa Mtwara-Mikindani imepokea fedha milioni 500 kutoka Serikali kuu kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu afya katika kituo cha afya Likombe. Miundo mbinu itakayojengwa katika mradi huo ni pamoja na Ujenzi wa Jengo la wodi ya mama na mtoto, Maabara, Nyumba ya mtumishi, Jengo la kufulia pamoja na Jengo la kulaza maiti.
Aidha Manispaa katika ujenzi wa majengo hayo imeongeza ujenzi wa njia za kupita kwa ajili ya kurahisisha upitaji wa wagonjwa na watoa huduma. Mradi huu umeanza kujengwa mwezi oktoba na utakamilika desemba 31,2017.
Mradi huu umejengwa na mafundi wenyeji kutoka eneo la Manispaa na kusimamiwa na Kamati ya afya ya Kituo kwa kushirikiana na Timu ya Menejiment ya halmashauri
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.