Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Brig. Jen Marco Gaguti awataka wananchi wanaofanya biashara sabasaba na maeneo mengine kuhamisha bidhaa zao na kuhamia soko la chuno.
Amesema kuwa tayari ofidi yake ishatoa maelekezo ya kutaka bidhaa zote kuhamia soko la Chuno na kwamba itasimamia kuhakikisha wafanyabiashara hao wanahamia sokoni hapo.
Gaguti ametoa maagizo hayo leo Mei 31, 2021 alipofanya ziara yake ya kwanza ya ukaguzi wa soko la Chuno pamoja na kuongea na wafanyabiashara wa soko hilo.
Katika kuhakikisha soko hili linaendelea kufanya kazi amewasisitiza wananchi wote wa Manispaa ya Mtwara –Mikindani kutumia soko la Chuno kupata huduma mbalimbali badala ya kutumia masoko mengine.
“Itakuwa ni dharau sana kwa Serikali imetuletea soko zuri halafu hatutaki kulitumia ni dharau kwa watanzania pia kwa sababu fedha hizi ni kodi ya wananchi tulitumie soko hili vizuri”Amesema Gaguti
Wakati huo huo Gaguti ameishukuru Serikali kwa kutoa shilingi Bilioni 5.3 za ujenzi wa soko hilo na kuwataka wafanyabiashara kutoa huduma iliyo bora na kuuza bidhaa bora ili kuwapata wateja badala ya kuamini Imani za kishirikina.
Aidha amewahaidi kuwapa ushirikiano wajasiri ya mali wadogo waliopo kwenye Mkoa wake ili waweze kufanya biashara kwenye mazingira mazuri na kuongezea kipato.
Hii ni ziara yake ya kwanza kufanya ndani ya Mkoa wa Mtwara tangu alipoteuliwa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan Mei 15 Mwaka huu.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.