Vikundi 59 vya wanawake, Manispaa ya Mtwara-Mikindani vimepatiwa mkopo wa asilimia kumi usio na riba awamu ya pili, jumla ya Shilingi milioni mia tatu sabini na tano mia tano arobaini na tatu (375,543,000) kutoka kwenye mfuko wa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu unaolenga kuwawezesha wananchi kiuchumi na kufanya Manispaa hiyo kufikisha shilingi bilioni moja milioni kumi na sita, mia tano ishirini na nane (1,016,528,000) zilizokopeshwa katika mwaka wa fedha wa 2024/2025.
Akizungumza Leo Juni 11,2025 katika Ukumbi wa Tilla, kwenye hafla fupi ya kukabidhi hundi ya mkopo huo, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani Mhe. Shadida Ndile amewataka wanawake hao kutumia fedha walizokopeshwa kuendeleza mitaji yao ili waweze kurejesha mkopo kwa wakati na vikundi vingine viweze kukopeshwa na kufaidika na mkopo huo.
“Sitegemei kuona hapo baadae tutakuja kukamatana, kunyang’anyana vitu na kupelekena polisi, ninaamini fedha hizi zitaenda kuinua mitaji yetu ili fedha zirudi na turejeshe mikopo yetu ili na wengine wakope tena” alisema Mhe. Ndile.
Amesema kuwa Manispaa haina ubaguzi kwenye utoaji wa mikopo kwa kuwa inazingatia kanuni, sheria na miongozo iliyowekwa, hivyo amewataka wanawake hao kuwa mabalozi kwa watu wengine ambao hawakufanikiwa kupata mikopo kwa awamu hii ili kuondoa dhana ya uwepo wa upendeleo kwenye zoezi hilo.
Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Bi. Juliana Manyama amewasisitiza wanawake hao kuwa wavumilivu na kuepuka kutumia lugha za matusi na kejeli kwa viongozi na Maafisa wanaohusika na mikopo pindi mchakato wa mikopo unapokuwa unaendelea kwa kuwa wahitaji ni wengi na fedha za ukopeshaji zinategemea na urejeshaji wa mikopo ya vikundi.
Akizungumza kwa niaba ya wanawake wenzake Bi. Jesca Masanja mkazi wa majengo amesema kuwa, wanatarajia mkopo huo utawanufaisha kiuchumi na kutoa wito kwa
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.