Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara-Mikindani leo 12 Mei, 2025 imekabidhi jumla ya vitimwendo (wheelchairs) 40 kwa watu wenye changamoto ya ulemavu ili kuwasaidia kujikwamua katika shughuli zao za kila siku.
Vitimwendo hivyo ni msaada toka shirika la kidini la 'Helping Hand' kupitia mradi wao wa 'Wheelchairs Distribution Tanzania 2025'
Akikabidhi msaada huo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Manispaa, Kaimu Mkurugenzi, Ndugu Mipawa Majebele amesema vitimwendo hivyo ikawe ni chachu kwa wao kuendelea kujiimarisha kijamii na kiuchumi kwani bado wanayo nafasi ya kufanya mambo makubwa licha ya changamoto yao ya ulemavu.
Kwa upande wake Afisa Mradi toka Helping hand, Hassan Kimbwembwe, amesema Shirika hilo la lilipokea maombi kutoka Manispaa ya Mtwara-Mikindani juu ya uhitaji wa Vitimwendo hivyo na wametekeleza ili kuwapa nafuu watu hao wenye changomoto mbalimbali za kijamii.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.