Idara ya Ardhi Manispaa ya Mtwara-Mikindani imekabidhiwa pikipiki mbili zenye thamani ya Shilingi milioni tano laki mbili (5,200,000) kutoka kwenye mapato yake ya ndani ili waweze kusimamia na kudhibiti ukuaji holela wa mji.
Akikabidhi pikipiki hizo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Manispaa, Mkuu wa Kitengo cha Mipangomiji na Ardhi, Rugembe Maiga amesema lengo la kuwapatia pikipiki hizo ni kuhakikisha wanasimamia vyema Wananchi wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani kuhakikisha wanazingatia taratibu za ujenzi mjini.
Maiga alitumiwa wasaa huo pia kuwashukuru Madiwani wa Manispaa ambao ndiyo walipendekeza ununuzi huo na amemshukuru Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani Mwalimu Hassan Nyange kwa kuridhia kutoa fedha za kununua pikipiki hizo ambazo zitawezesha wataalamu kufanya ukaguzi wa mara kwa mara ili kudhibiti ujenzi holela na kuhakikisha kuwa ujenzi wowote unaofanyika ndani ya Manispaa unakidhi matakwa ya kisheria kwa kuwa na nyaraka za umiliki (Hatimiliki) na kibali cha ujenzi.
Vilevile amesema Kufuatia kupatikana kwa pikipiki hizo kutapunguza kwa kiasi kikubwa migogoro ya ardhi ikiwemo migogoro ya uvamizi wa maeneo ya Umma na migogoro ya kutotii sheria zinazosimamia masuala ya uendelezaji wa ardhi kwani wataalamu sasa wataweza kuzunguka maeneo mengi zaidi.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.