Mkuu wa Idara ya Elimu Msingi, Manispaa ya Mtwara-Mikindani, Bi. Optuna Kasanda, amewataka walimu kuwa viongozi, walezi na 'walinzi' wazuri kwa wanafunzi hasa wa kike kwa kuwapa miongozo sahihi itakayowaepusha na kujihusisha na tabia hatarishi zinazoweza kuwaharibia masomo.
Ameyasema hayo wakati wa kufunga mafunzo ya ufafanuzi wa kanuni za maadili ya utendaji kazi katika Utumishi wa walimu yaliyohusisha walimu wakuu wote wa Halmashauri ya Manispaa Mtwara.
Mafunzo hayo ni sehemu ya utekelezaji mpango wa Serikali wa mradi wa uboreshaji wa Elimu ya Awali na Msingi (BOOST) yamefanyika katika ukumbi wa Chama Cha Walimu (CWT) Manispaa ya Mtwara-Mikindani.
Bi. Kasanda pia aliwahimiza Walimu Wakuu hao kufanya usimamizi mzuri na kukarabati miundombinu ya shule kama madawati yaliyoharibika, ili kujenga mazingira rafiki kwa wanafunzi.
Aidha, amesisitiza shule kudumisha na kuzingatia Usafi wa mazingira ya shule hususani madarasani na vyooni ili kuepukana na maradhi ya mlipuko.
Sambamba na hayo aliwataka Walimu kuendelea kutilia makazo taaluma na hasa katika madarasa ya awali ili wanafunzi waweze kuelekea vyema Stadi za Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK).
@tumeyautumishiwawalimu
@wizara_elimutanzania
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.