WATENDAJI WAMETAKIWA KUFANYA KAZI KWA KUFUATA SHERIA.
Watendaji wa Halmashauri wametakiwa kufanya kazi kwa bidii na kwa kufuata sheria,taratiibu, kanuni na miongozo inayotolewa na Serikali na kuacha kusingizia siasa kama kikwazo katika utendaji wa kazi zao na utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.
Hayo yamesemwa jana tarehe 7 April 2017 na Mwenyekiti wa Alat Mkoa wa Ruvuma Mh: Daniel Nyambo kwenye kikao cha majumuisho cha ziara ya siku mbili kilichofanyika katika Ukumbi wa Manispaa Mtwara Mikindani.
Bwana Nyambo Alisema kuwa suala la watendaji kuacha kufanya kazi na kusingizia wanasiasa kwamba wanawakwamisha sio la ukweli,amewataka wafanye kazi kwa kuwa wameapa kufanya kazi na wanalipwa mshahara kila mwezi kwa kazi zao.
“Acheni vizisingio fanyezi kazi kwa kufuata kanuni, taratibu, sheria na miongozo maswala ya siasa waachieni wanasiasa” alisema.
Aidha Mwenyekiti huyo aliishauri Manispaa Mtwara Mikindani kutilia mkazo suala la ukusanyaji wa mapato kwa kuwa wafanyabishara wengi hawako tayari kulipa kodi mbalimbali, alishauri sheria ndogondogo zitumike katika ukusanyaji wa mapato.
Nae Mtsahiki Meya wa Manispaa ya Songea Mh: Abdul Shaweji aliwashukuru wataalamu kutoka Manispaa kwa kuwapokea vizuri na kuwapa ushirikiano mkubwa, na kusema kuwa wamejifunza mengi, lakini alisisitza kuendelea kushirikiana baina ya Manispaa hizi mbili ikiwa ni pamoja na kujenga tabia ya wataalamu kutembeleana ili kujengeana uwezo utakaoimarisha utendaji wa kazi.
Mstahiki Meya wa Manispaa Mtwara-Mikindani Mh: Geofrey I. Mwanichisye aliwaomba watu wa Mkoa wa Ruvuma kujiona kuwa nao wapo Kusini na kwamba kuna forum ya uwekezaji ya Lindi na Mtwara ni vema Mkoa wa Ruvuma nao wakashiriki ili kuitangaza kusini.
Aidha amewashukuru wageni kwa Ujio wao na kuwaeleza kuwa Manispaa Mtwara-Mikindani tuko imara katika utendaji wa kazi na tunatekeleza kauli ya Mh. Rais ya HAPA KAZI TU.
“Sisi tuko imara na tunatekeleza ahadi ya hapa kazi tu bila ya kujali itikadi ya vyama vyetu”alisema.
Ziara hiyo iliyoanza kuanzia tarehe 6-7 April 2017 ilikuwa na lengo la kujifunza na kujengeana uwezo kuhusu uendeshaji wa shughuli mbalimbali za Halmashauri ikiwa ni pamoja na Kujifunza ukusanyaji wa mapato pamoja usafi wa mazingira.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.