Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Dustan Kyobya amewataka Madiwani na Watendaji wa Mitaa Manispaa ya Mtwara-Mikindani kuanzisha na kuboresha vikundi vya ulinzi shirikishi katika Kata ili kuimarisha ulinzi na usalama katika maeneo yao.
Mhe.Kyobya amezungumza hayo Agosti 1, 2021 katika Mkutano maalumu wa Baraza la Madiwani uliofanyika katika Chuo cha ualimu (TTC).
“Waheshimiwa Madiwani na watendaji wa Mitaa shirikianeni katika kuhakikisha zile changamoto ambazo zinahatarisha amani yetu tunazitatua mapema kwa kuanzisha na kuimarisha vikundi vya ulinzi shirikishi katika maeneo yetu”Amesema Kyobya
Amesema kuwa maendeleo yoyote yanawezekana endapo kuna hali nzuri ya usalama katika eneo husika, hivyo amewata Madiwani na Watendaji kwa kushirikiana na wananchi kuunda vikundi vitakavyoimarisha ulinzi katika Kata.
Pamoja na hayo, Mhe Kyobya amewataka Madiwani kuhamasisha wananchi juu ya ujio wa mwenge katika Mkoa wa Mtwara pamoja na kuendelea kutoa elimu kwa wananchi jinsi gani ya kujikinga na UVIKO 19 hasa katika kipindi hiki cha mapokezi ya mwenge katika Mkoa wa Mtwara.
‘Mwenge utapokelewa tarehe 28 mwezi wa nane pale Mpapura ukitokea Lindi, tukawe mabalozi wa kuhakikisha kwamba mwenge tunaupokea vizuri lakini pia tusisahu kutoa elimu juu ya UVIKO 19, tuupokee mwenge huku tukichukua tahadhari zote” Amesema Mhe.Kyobya
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.