Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe.Mwanahamisi Munkunda amesema kuwa Serikali kupitia wakala wa Barabara za vijijini na mijini (TARURA) inatarajia kuanza ukarabati wa miundombinu ya barabara zote korofi zilizopo Manispaa ya Mtwara-Mikindani zilizoharibiwa na Mvua za Elnino na kimbunga hidaya.
Amesema kuwa Fedha za ukarabati wa barabara hizo tayari zimefika hivyo kuanzia mwezi Agosti mwaka hu wakandarasi wataanza kazi.
Aidha amewataka waheshimiwa Madiwani kuambatana na wataalamu kufanya Mikutano katika maeneo yao kuwajulisha wananchi makubaliano ya baraza hilo juu ya ukarabati wa barabara.
Vilevile Munkunda amezipongeza kamati mbalimbali za halmashauri zilizoteuliwa katika mkutano huo na kuzitaka kufanya kazi ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi huku akiwasisitiza Madiwani kuhakikisha miradi ya maendeleo inakamilika kwa wakati ili isaidie kujibu kero za wananchi.
Kuelekea kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Mwezi Oktoba Mwaka huu,Mkuu wa Wilaya amewataka waheshimiwa Madiwani wa Manispaa kuendelea kuhamasisha wananchi hususani Vijana kupitia michezo mbalimbali kwa kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura na kuweza kuwachagua viongozi wazuri wanaowahitaji.
Hayo yamezungumzwa Leo Agasti 1,2024 katika Mkutano wa balaza la madiwani la robo ya nne la kujadili taarifa za Halmashauri kwa kipindi cha Mwaka 2023/2024 uliofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara (boma)
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.