Wajumbe wa baraza la Madiwani Manispaa ya Mtwara-Mikindani kwa pamoja wameidhinisha taarifa ya hesabu za halmashauri za mwaka wa fedha wa 2021/2022 zinazoishia Tarehe 30/6/2022 ili taarifa hiyo iweze kukabidhiwa kwa Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa hesabu za Serikali (CAG) .
Taarifa ya hesabu za halmashauri inahusisha taarifa mbalimbali za halmashauri (Council Information), Ripoti ya halmashauri ya hesabu za mwaka 2021/2022 (Report of those Charged with governance), taarifa ya hesabu za mwaka 2021/2022 (Fianancial statement) pamoja na mchanganuo wa taarifa ya hesabu za mwisho (Notes to the Financial Statement).
Pamoja na kuidhinisha taarifa hiyo Mstahiki Meya Shadida Ndile amewahimiza madiwani kila mmoja kwenye eneo lake afuatilie miradi ya maendeleo inayotekelezwa na pale anapoona pana changamoto asisite kuwasiliana na Mkurugenzi kwa ajili ya ufafanuzi.
Aidha amemuagiza Mkurugenzi kumtafuta mtaalamu atakaefanya kazi kwenye chumba cha maiti (mortuary) iliyopo Kituo cha afya Likombe ili huduma zianze kutolewa.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.