Wajumbe wa baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara-Mikindani wameridhia na kupitisha rasimu ya mpango na bajeti ya mwaka 2023/2024 ambapo Manispaa imekadiria kukusanya na kutumia shilingi bilioni thelathini milioni mia moja thethini na mbili laki mbili sabini na moja mia nne na tatu (30,132,271,403.00) kutoka katika vyanzo mbalimbali vikiwemo vya mapato ya ndani.
Akiwasilisha bajeti hiyo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara- Mikindani , Mkuu wa Divisheni ya Mipango na takwimu Gwakisa Mwasyeba amesema kuwa Manispaa inatarajia kukusanya shilingi (5,445,000,000) kutoka kwenye mapato yake ya ndani, ruzuku ya matumizi mengineyo (840,688,200), ruzuku ya mishahara (15,792,162,200.00), Ruzuku ya miradi ya Maendeleo kutoka Serikalini (5,627,920,497.00) pamoja na ruzuku ya miradi ya maendeleo kutoka kwa wahisani (2,426,500,506)
Kwa upande wa matumizi Mwasyeba amesema kuwa Manispaa imepanga kutumia shilingi bilioni tisa milioni mia tisa laki nne ishirini na moja na elfu tatu( 9,900,421,003. 00 ) kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo ambapo kati ya hizo shilingi bilioni moja milioni mia nane arobaini na sita (1,846,000,000.00) ni fedha kutoka katika mapato ya ndani ya halmashauri zikijumuisha fedha za mfuko wa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu shilingi milioni mia nne sitini na moja laki tano (461,500,000), fedha za ruzuku ya Maendeleo kutoka Serikali Kuu shilingi bilioni tano milioni mia sita ishirini na saba laki tisa ishirini mia nne tisini na saba (5,627,920,497.00) na fedha kutoka kwa wahisani shilingi milioni mbili milioni mia nne ishirini na sita laki tano mia tano na sita (2,426,500,506) .
Amesema kuwa katika utekelezaji wa bajeti hiyo Manispaa imejielekeza katika vipaumbele mbalimbali vikiwemo kusimamia na kuimarisha ukusanyaji wa mapato ya ndani, Kuboresha upatikanaji wa huduma zenye ubora kwa jamii (elimu afya, maji barabara, mawasiliano n.k), uboreshaji wa ustawi wa Maisha ya wananchi, kutenga maeneo kwa ajili ya kufanya biashara kwa wajasiariamali, ugawaji wa rasilimali kwenye miradi ya kielelezo kwa ajili ya maendeleo ya viwanda pamoja na vipaumbele vingine vingi.
Aidha ameishukuru Serikali Kuu kwa kuendelea kuipatia Manispaa ruzuku ya kulipa mishahara ya watumishi, matumizi mengineyo na miradi mbalimbali ya maendeleo Pamoja na kuwashurukuwadu mbalimbali waliowezesha Halamshauri katika kuekeleza majukumu yake.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.