Baada ya Menejimenti kufanya mchakato wa kutunga sheria ndogo saba za halmashauri ya Manispaa ya Mtwara-Mikindani za mwaka 2022 kwa kuziboresha ziliziopo na kutunga nyingine mpya , Oktoba 7,2022 Baraza la Madiwani la Manispaa ya Mtwara-Mikindani limeridhia na kupitisha rasimu ya sheria ndogo hizo ili zipelekwe kwa Waziri mwenye dhamana ya Serikali za Mitaa kwa ajili ya kuzisaini na kuchapishwa kwenye gazeti la Serikali na baadae zianze kutumika.
Shreria ndogo zilizopitishwa ni pamoja na sheria ndogo za uanzishaji wa mfuko wa afya ya jamii ulioboeshwa, Sheria ndogo za afya na usafi wa mazingira, sheria ndogo za Kilimo na Usalama wa Chakula.
Sheria nyingine ni pamoja na sheria ndogo ya ujenzi mjini, sheria ndogo za ada na ushuru, sheria ndogo za usimamizi wa masoko pamoja na sheria ndogo za Mji Mkongwe wa Mikindani.
Mchakato wa utungaji wa sheria ndogo hizi ulianza mwezi Januari mwaka huu kwa kukusanya maoni na mapendekeo kutoka kwa wananchi pamoja na wadau wengine wa Maendeleo
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.