Baraza la Madiwani, Halmashauri ya Manispaa Mtwara-Mikindani leo tarehe 23 Mei, 2025 imefanya ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo iliyochaguliwa na Halmashauri ya Manispaa kwa ajili ya kukaguliwa, kuwekewa jiwe la msingi na kuzinduliwa na Mwenge wa Uhuru hapo Jumapili (25/05/2025).
Likiongozwa na Naibu Meya, Mhe. Sixmund Lungu, Baraza limetoa maboresho madogo katika miradi inayohitaji kuboreshwa zaidi na wamepongeza juhudi na jitihada za Manispaa kwenye uchaguzi wa miradi.
Tarehe 25/5/2025 Mwenge wa Uhuru Utapokelewa katika eneo la Soko la Milumba majira ya saa 1 asubuhu na Mkesha utakuwa katika Viwanja vya Sabababa, ambapo Msanii Shoro Mwamba na wengine wengine watatumbuiza siku hiyo.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.