Baraza la Madiwani la Manispaa ya Mtwara-Mikindani lililoketi Leo Machi 1, 2024 limeridhia na kupitisha rasimu ya mpangp na bajeti ya mwaka wa fedha wa 2024/2025 Shilingi Bilioni thelathini na tatu milioni mia moja tisini na mbili laki moja elfu hamsini na mbili (33,192,152,000) ambayo imebeba matamanio ya wananchi wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani na imegusa kila sekta
Akiwasilisha taarifa ya mpango huo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani, Mkuu wa Idara ya Mipago, Takwimu na Ufuatiliaji , Gwakisa Mwasyeba amesema kuwa katika bajeti hiyo Halmashauri imekadiria kukusanya Shilingi bilioni tano milioni mia nne kumi na tisa mia moja arobaini na saba elfu (5,419,147,000) kutoka katika mapato yake ya ndani, Ruzuku ya matumizi mengineyo (Other Charges) Shilingi milioni mia tisa thelathini na nane mia saba na kumi elfu (938,710,000), Ruzuku ya mishahara Shilingi bilioni kumi na tisa milioni mia sita na sita laki moja kumi na sita elfu (19,606,116,000), Ruzuku ya miradi ya maendeleo kutoka Serikali Kuu Shilingi bilioni nne milioni mia saba arobaini na tisa laki tatu thelathini na tatu (4,749,333,000) pamoja na ruzuku ya miradi ya maendeleo kutoka kwa wahisani Shilingi bilioni mbili milioni mia nne sabini na nane laki nane arobaini na sita elfu (2,478,846,000).
Kwa upande wa matumizi amesema kuwa Manispaa ya Mtwara-Mikindani imepanga kutumia Shilingi bilioni thelathini na tatu milioni mia moja tisini na mbili laki moja hamsini na mbili elfu (33,192,152,000) ambapo Shilingi bilioni tano milioni mia nne kumi na tisa laki moja arobaini na saba (5,419,147,000) zitatoka katika mapato ya ndani, Shilingi Bilioni saba milioni mia mbili ishirini na nane laki moja sabini na tisa elfu (7,228,179,000) fedha za miradi ya maendeleo kutoka Serikali Kuu , Shilingi bilioni kumi na tisa milioni mia sita na sita laki moja kumi na sita elfu (19,606,116,000) zitatumika kulipa mishahara pamoja na shilingi milioni mia tisa thelathini na nane laki saba na kumi (938,710,000 )za matumizi mengineyo (OC).
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.